Viongozi wa Vilabu msipo badiilika kwenye hili mjue mtazidi kulishusha soka la Tanzania

Viongozi wa Vilabu msipo badiilika kwenye hili mjue mtazidi kulishusha soka la Tanzania

brave_3

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2014
Posts
1,186
Reaction score
705
Leo katika kukaa kwangu nika jaribu kuvuta picha kwa matukio madogo madogo yanayo tokea ndani ya soka letu la Tanzania kiujumla Nasio kwa Ngazi ya ligi kuu tu bali hata mitaani huku ambako soka lina anzia..........

Nataka nizungumzie swala hili ambalo kwa siku za hivi karibuni halijaguswa kabisa...swala la kutumia UCHAWI au NGUVU ZA GIZA kwenye soka..Siku kadhaa zilizo pita katika uwanja wetu mpya inasemekana walikuta vitu ambavyo vilikuwa viki husishwa na imani za kishirikina......

Nikawa najiuliza je kweli nguvu hizi bado zina nafasi katika soka letu la Tanzania kwa sasa? bado akili yangu ina niambia hapana..Najiuliza hivi ni kweli TFF wameshidwa kuyazuia haya mambo yanayo tokea katika soka letu? natumai kuna kanuni na sheria zake katika kuhusu hili.. Kwanini hivi vitu viki fanyika uwanjani na vikionekana lakini hakuna hatua zozote zinazo chukuliwa..TFF pasipo kujua hili swala lina fanya soka letu la Tanzania lizidi kuzorota siku baada ya siku......!

Ninategemea kwa msimu huu kuona baadhi ya timu kufata nyayo za MBAO FC . Ukiniamsha leo ukaniambia kwa mwaka jana ni timu gani iliyo fanya vizuri nitakwambia ni mbao.. ni timu iliyo jipanga kwa kweli achilia mbali KAGERA SUGAR..Timu iliyo na vijana wenye nguvu na kujituma sasa kwanini Timu zingine zisitengeneze timu bora ambayo ipo watajua inaweza kupambana na Timu pinzani...kuliko kutegemea mambo ya kishirikina...

Kuna muda wa Tanzania hatupaswi kumlaumu kocha wetu timu ya Taifa kufanya vibaya..Tuvilaumu vilabu vyetu kuwa na mifumo mibaya na njia za ujanja ujanja katika kupata matokeo mazuri..Tuseme ukweli Soka letu lipo mahala pazuri kwa sasa ila watao lipeleka upande ni vilabu vyenyewe....!

kwa kumalizia : TFF lazima muwe makini watanzania tuna waamini sana mnaweza lipeleka soka letu kunako takiwa..TFF mjue ya kuwa Kinacho uwa soka letu na kufanya kukosa mvuto ni USHIRIKINA na RUSHWA NDANI YA UWANJA NA NJE YA UWANJA mkiweza kujikita kwenye hivyo vitu soka letu litapiga hatua..Nasheria sikate pande zote iwe Simba au Yanga au hata Mtibwa sugar pasipo kujali nani mkubwa na nani mdogo...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom