Viongozi wa Yanga heshimuni sheria ya mavazi kwa kocha wenu

mpimamstaafu

JF-Expert Member
Joined
Jul 18, 2018
Posts
4,445
Reaction score
4,707
Hakika inashangaza sana kuona Viongozi wa Klabu ya Yanga na WAPENZI wa Klabu hiyo wanagomea sheria ya mavazi iliyotolewa na TFF.

Watanzania sio nchi ya wahuni,kiongozi kama Kocha lazima uvae mavazi ya heshima kama suti,track sute au hata shati na suruali.

Kitendo cha Kocha kuvaa vipensi sio sahihi ,vipensi ni mavazi ya kihuni.Tanzania ni nchi yenye kuheshimu Maadili. Tunaushauri Uongozi wa Yanga uheshimu sheria ya mavazi kwa Kocha wao.
 
miaka yoote walikuwa wapi leo wamuone ZAHERA ndo walete hizo sheria zao?
 
miaka yoote walikuwa wapi leo wamuone ZAHERA ndo walete hizo sheria zao?
Sheria mpya hiyo mkuu hiyo miaka ya nyuma haikuwepo sasa wangemhukumu vipi aache mavazi ya kihuni
 
Da! Simba ni mbumbumbu kiutani kwa watani Lkn gongo wazi ni mbumbumbu wa akili yaani ni weupe kichwani hadi wanatia aibu
 
Hivi juzi benchi la ufundi la taifa stars vs Burundi walivaaje
 
Tff wanaleta sheria mpya na inatumika kwa yanga tu.
Mbona ndairagije mechi ya ngao ya jamii alivaa bukta na hakuchukuliwa hatua yoyote?
Sheria yenyewe imekaa kikuda tu unatamka mavazi nadhifu na ya heshima lakini haitamki mavazi hayo ni yapi?
 
Yanga wasipodhibitiwa watavaa chupi
Hivi Kwanini hii sheria imuwajibishe kocha pekee yake ndio avae nguo nadhifu kwa maana ya kutovaa vibukta lakini sheria hiyo hiyo kwanini haikuwagusia wachezaji na marefa rii ambao vazi lao kubwa wanapokuwa uwanjani ni bukta. Jezi zile ndio zimekosa unadhifu kabisaa maana zinacholesha sana hasa upande wa mbele na isitoshe wakati mwingine mchezaji hudondoka hadi kupelekea paja lote liwe wazi. Sasa kama TFF wanania ya kuleta unadhifu uwanjani, kwanini wasiwaambie na wachezaji pamoja na marefarii wavae nguo nadhifu pia?
 
Hayo magazine unayoyataja umeyanukuu kutoka Kifungu gani cha hiyo Kanuni unayoisema?
 
Nakusudia hayo mavazi umeyanukuu kwenye sehemu gani ya hiyo Kanuni unayoisema?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…