Viongozi wa Yanga kuweni makini, msije kukurupuka mkamsajili Chama

Kilichoibeba yanga ni umoja wa wachezaji wote msimu mzima, hakuna aliyekua anaonyesha yupo juu kuliko mwingine, sikatai Chama ni mchezaji mzuri ila atakuja kuvuruga dressing room ya timu na morali,
Huu ndio ukweli, huyu ni mchezaji anayetaka u father na Yanga ilikuwa imeshatoka huko. Embu angalia Azizi Ki na Pacome pamoja na ubora na kiwango chao kikubwa lakini wana upendo na kila mtu na wanatamani kila mmoja aonyeshe kiwango.
 
Nani kakwambia Yanga wanamtaka Chama?,Yanga wanachofanya ni kuwazidishia Presha Simba ili waendelee kuwang'ang'ania magarasa yao ili wembe uwe ni ule ule!

Chama hana Umuhimu kwasasa pale Yanga!
Sema kweli?
 
Hata mimi nitawashangaa sana Yanga kama wataendelea kuokoteza wachezaji kama Chama, Baleke, au Moses Phiri!!
Sura mpya kama zile za akina Aziz Kii ndiyo kila kwenye mafanikio makubwa ya Yanga.
Kwahiyo umeanza kuwashangaa Yanga au unajishangaa mwenyewe?
 
amekubali hamumtaki tena mmemtongoza weee
 
hofu yangu ni kuwa, ameshasajiliwa, ila alishakuwa na mazungumzo na simba moo, asijekuwa amesaini, atakuwa anacheza ila anakula kote ili asaboteji, akijulikana anafanya hivyo awekwe bench miaka yote miwili. bora tumlipe mshahara wa bure.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…