Viongozi wa yanga zingatia

fimboyaasali

JF-Expert Member
Joined
Jan 14, 2011
Posts
8,617
Reaction score
8,244
haya ni mambo muhimu sana kwa maendeleo ya yanga ndani ya miaka 10 ijayo:
1.kujenga uwanja
2.kumnunulia gari kila mchezaji
3.kununua ndege kwa ajili ya usafiri
4.kujenga sanamu ya tabu mangara tabu makao makuu ya yanga
5.kuanzisha maduka ya kuuza bidhaa za yanga nchi nzima
6.kushirikiana na azam tv kuitangaza yanga dunia nzima
7.kuanzisha timu ya yanga kwenye kila nchi afrika mashariki
5.
 
Wafanye hayo yote kwa mapato yapi wanazoingiza?
 
Kwanza Yanga inabidi muhame pale Jangwani mmejenga bondeni. Kuna siku kale kajengo kenu tutakakuta Kunduchi baharini.
 
Watu kama wwwe mnafanya washabiki wa mpira tunadharaulika sana. Kama ningekua kiongozi wa Yanga kati ya mambo nisingeyapa kipaumbele ni swala zima la ujenzi wa uwanja. Ni heshima timu kuwa na uwanja wake ila kiuhalisia hamna faida kubwa kumiliki uwanja.
 
Kwa Tanzania viwanja vya mpira havina faida kwasababu ya mfumo wa unyonyaji wa TFF. Makato kibao
 
Kweli kabisa uwekazaji mkubwa uwe kwenye facilities nyingine mfano Gym ya kisasa, uwanja wa mazoezi mzuri na hostel zakisasa Ac Milan na intel milan mpk leo hawana viwanja
 
Njia pekee ya kuitangaza timu ni kuendelea kushiriki michuano ya kimataifa na kuchukua makombe ya kimataifa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…