Viongozi wafikishwa polisi kwa kuwahadaa wanachuo wa CBE na DIT

mpenda pombe

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2010
Posts
1,406
Reaction score
711
Muda huu nipo kituo cha salenda bridge.. Mara wanafika wanafunzi wa CBE na DIT Pamoja na watuhumiwa wao, wanadai waliahidiwa kupewa posho ya shs 10000/= wakienda uwanja wa uhuru kushuhudia sherehe za uhuru wa tanganyika... Sasa imegeuka ahadi hewa hawajapewa hela yeyote..

My take...
Kwa tukio hili Thamani ya wasomi inazidi didimia
 
Hii si ishara nzuri, inaonyesha jinsi watu wasivyo tayari kwa ajili ya nchi yao mpaka walipwe kuifanyia jambo.
Si kosa lao, ni mfumo ndivyo umewafanya, walipwe tu.
 
Kutokubalika kwa watawala ndio kikwazo cha uzalendo.

Utaenda kumshagilia na kumwangalia nani iwapo yeye mwenyewe hajijuwi, hatake care, anatukana watanzania rejea ya wafanyakazi nitawapiga na sizitaki kura zenu (hawa ni watoto na wale ni wazazi) Wanapata mimba kwa vihelehele vyao
ahadi nyingi zisizotekelezeka, kushindwa kuoenesha huruma na kushindwa kutekeleza utawala bora nk.

Hayo yote ukiyakusanya yanaenda kuharibu uzalendo wa watu, na serikali kuogopa kuumbuka inabidi kutoa hongo kuwapata watazamaji. (hii ni ruswa, ni njia ya chama tawala ccm kila siku kuhonga pilau, fedha na mavazi na sasa serikali imeingia mkenge)
 
UMENENA VEMA MKUU! niache kazi zangu niende kumwangalia yule bwana wa magogoni anachekacheka tu huku nchi inazidi kudidimia kwa umasikini, rushwa, kutapakaa kwa madawa ya kulevya, afya mbovu elimu mbovu, usalama wa raia mashakani, chuki za kidini zikizidi kushika kasi wakati nyumbani watoto hawana chakula! NI UPUUZI.....HAYA MAMBO NDO YANAYOTUFANYA TUSIONE UMUHIMU WA SHUGHULI NA SIKU KAMA HIZI.....HATA kwenye tv sipotezi muda wangu kuangalia matusi yao
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…