Beatrice Kamugisha
JF-Expert Member
- May 18, 2019
- 762
- 6,984
Kwa umri wetu tunaona mengi, kiongozi anapofanya kampeni usaidiwa na watu mbalimbali na wengi uwalipa fadhila ya ajira.
Ntatoa mfano, Yule kijana Nassary wa Arusha ameahidiwa ajira, ili apate hiyo ajira lazima Kuna mtu atapoteza ajira. Hi ni ishara ya namna watu wanavyoadhibiwa na wanasiasa baada yakumaliza kampeni.
Nirudi kwenye hoja, asilimia zaidi ya 70 ya viongozi wa vyombo vya dola walioshiriki kwa nguvu kubwa kuuweka utawala wa awamu ya Tano walitumbuliwa na baadhi kupangiwa kazi nyingine...awakutumbuliwa kimyakimya Bali waliondolewa kwa kashfa na tuhuma mbele ya vyombo vya habari na barua ya Msigwa juu. Hivyo hata vitukuu vyao vinatambua walitumbuliwa.
Hii ni pamoja na wakurugenzi na viongozi wengine wengi. Baadhi Hadi leo wapo ndani na kesi zao hazijaanza kusikilizwa.
Kwanini nayasema haya, nawakumbusha viongoz wa vyombo vya dola kwamba upo uwezekano wasipotenda haki wakalazimisha matokeo ya mfukoni kwa kufuata maelekezo ya mtu mmoja, mtu huyohuyo akiaposhwa atakuwa wa Kwanza kukutumbua na kumweka mtu anayeona Leo anamfaa.
Bora ukasimamia haki hata ukitumbuliwa utarudi uraiani tutakupokea, ila ukionyesha mwingi wa amri na machukizo kwa wananchi, ukasababisha wenye haki wawe vilema na baadhi yao kupoteza maisha unajiandalia maisha magumu utakapokua mwenyewe nyumbani bila kazi. Utakua na muda mwingi wa kusoma magazeti na habari zilizopita na mpya, habari hizo zitakukumbusha uovu wako . Hautasitirika.
Mliojaliwa kuwa na wazazi waliopo madarakani na makazini Sasa, wakumbusheni kutenda haki maana siku si nyingi madaraka yao yatapotea, watabaki raia wa kawaida. Muulizeni Naibu katibu mkuu wizara ya elimu alifanywa Nini kwa kosa gani!
Ogopa kumwaga dawa ya walipa Kodi kwa kutii amri, ukimwaga damu hakuna anayekupa nishani isipokuwa wataendelea kukupa kazi ngumu na watakuwa wanakutenga wakiamini ipo siku hata wao utawamwaga damu. Tusimamie haki