Viongozi wanafanya ufisadi wanapo pata madaraka kwasababu ya kuendekeza starehe

Viongozi wanafanya ufisadi wanapo pata madaraka kwasababu ya kuendekeza starehe

EllySkyWilly

JF-Expert Member
Joined
Aug 28, 2020
Posts
2,204
Reaction score
2,085
Tafadhari rejea kichwa cha habari hapo juu,

Viongozi wanafanya ufisadi mara wanapo pata madaraka kwasababu ya kuendekeza sitarehe mara baada ya kurubuniwa.

Hiki ndicho nachokifahamu wakuu, na wanao warubuni viongozi wetu mameneja wetu mpaka wanaanza kuwa wezi ni wanawake.

Meneja anadanganywa na mwanamke mpaka anafikia hatua ya kuanza kuiba pesa za kampuni au taasisi.

Waziri anapewa madaraka leo kesho pesa zinapotea wizarani kwanini kalewa anasa za mapenzi huyo.

Haina haja ya kutafuta mchawi ni kumsimamisha kazi na kumny'ang'anya mali zake zote.

Mara baada ya hapo nanukuu andiko kutoka kwenye kitabu cha Mithali 31, kinaelezea jinsi kiongozi anatakiwa kuwa ili asije akapotea katika uongozi wake.

Hapa neno mfalme linasimama badala ya kiongozi, au meneja au hata mtu wa kawaida anayeongoza maisha yake.

Mithali 31

1 Maneno ya mfalme Lemueli; mausia aliyofundishwa na mama yake.

2 Ni nini, mwanangu? Tena ni nini, mwana wa tumbo langu? Tena, ni nini mwana wa nadhiri zangu?

3 Usiwape wanawake nguvu zako; Wala moyo wako usiwape wale wawaharibuo wafalme.

4 Ee Lemueli, kunywa mvinyo hakuwafai wafalme, hakuwafai wafalme; Wala haifai wakuu waseme, Ki wapi kileo?

5 Wasije wakanywa na kuisahau sheria, Na kuipotosha hukumu ya mtu aliye taabuni.

6 Mpe kileo yeye aliye karibu na kupotea; Kampe divai yeye aliye na uchungu nafsini.

7 Anywe akausahau umaskini wake; Asiikumbuke tena taabu yake.

Naomba niishie hapo.
 
Back
Top Bottom