Viongozi wangu wa Simba ongezeni sana jitihada kwenye kamati za ufundi kama wanavyofanya Yanga, leo Azam ametoka sare wakati sisi katukomalia

Mwishokambi

JF-Expert Member
Joined
Nov 23, 2020
Posts
390
Reaction score
1,425
Mechi ambazo tunatoka sare unaona kabisa tumezidiwa mambo ya nje ya uwanja na nina wasiwasi sana kuelekea tarehe 8, tulikomaliwa na Fountain Gate kwa mambo ya nje ya uwanja, Azam naye akatuwekea ngumu kwa kusaidiwa na utopolo,

huwa mara nyingi sana Azam wanaombaga msaada utopolo wakitaka kuikabili Simba, nakumbuka nusu fainali ya Simba vs Azam kule Mtwara nilikuwepo, waganga wa utopolo ndio waliisaidia sana Azam wakishirikiana na watu wa Lindi, waganga walitokea Mtwara na Lindi, mechi ile Simba tulitolewa na Azam kwenye nusu fainali, mara nyingi mechi za Simba vs Azam ukiona sare ya 2 kwa 2 ujue mipang nje ya uwanja ilifanyika na kwetu haijakaa vizuri.

Wenzetu Utopolo wako kazini sasa hivi ili kutumaliza tarehe 8, wanasema wenyewe wajinga wajinga wao kuwa mpira unachezwa uwanjani lakini sio kweli, ndio maana wamefichuliwa siri zao kuwa hawaachi kwenda Pangani.

Leo Azam ametoka sare na Namungo pale Chamazi, lakini Azam yule ndio katuchomolea goli dakika za lala salama, huyu Azam hatatoka salama kwa Yanga.

Ushauri wangu lazima tujipange tuwe na watu wakatili, watu wetu wanaopewa kazi pia sio waaminifu, njaa zinawafanya wauze ishu zote, sio ajabu hata gemu na Yanga wanavujisha kila jambo.

Nimeumia sana leo.
 
Yanga ina namba 10 wafuatao.

1. Azizi ki.
2. Pakome.
3. Max
4. Chama.

Simba Ina nani??????

Kama Mpira Ingekuwa Uchawi Nigeria angekuwa Bingwa wa Kombe la Dunia wa Muda wote.

Kamuulize Mobutu alipeleka waganga wangapi kwenye Kombe la Dunia kule Germany 1974.

MADA ZA UGANGA NA MPIRA NAONA NI UPUMBAVU ULIOPINDUKIA.
 
HUU NDIO UFUNDI SIMBA INAPASWA KUFANYA SAJILI ZA MABORESHO ZISIZOPUNGUA TANO.

TIMU BADO SANA KUFIKA WALAU NUSU WA ILE YA 2019.

WAACHANE NA.
1. Joshua Mutale.
2. Karabue Chamoe.
3 .Agustine Okejepha.
4. Dese Mukwala.
5. (Ngoma).
6 Manula.

MABORESHO YA SAJILI.
Beki wa kati NO 5.
Kiungo mkabaji No 6.
Kiungo mshambuliaji 10.
Mshambuliaji No 9.

Hadi leo sijapata majibu kwanini Fadru alisajili mchezaji mmoja tu Dirisha Dogo, ilinishangaza sana!!!!!!!!

Au ndio kuvizia ma Free Agent.

HUU NDIO UFUNDI MZEE
 
Yanga Mnanishangaza!Hivi Ni Nini Kinapelekea Kupita Milango Isiyo Rasmi Ikiwa Mpila Ni Uwanjani?
 
Mpira unachezwa uwanjani, wewe unaleta mambo yako ya kishirikina.

Inasikitisha kua na watu wa aina hii Azam huyu huyu alimfunga Yanga na akasababisha beki wa Yanga kupata kadi nyekundu,Je hao waganga wanaomsaidia Azam kushinda au kumdhibiti Simba wanaoletwa na Yanga waliamua kumsaliti Yanga na kua upande wa Azam?
 
Fatilia mpira we kijana! Azam ana sare nyingi sana yani huo ni muendelezo tu wa sare..
Amesare na Coast nyau nyau! Kasare na Simba 2 - 2
Kasare jana na Namungo
Tabora united hali kadhalika
 
Niliwahi kuandika siku moja kuwa hili jukwaa ili liwe na hadhi inatakiwa ufanyike mchujo maalumu wa kuchangia au kuleta mada...ila kwahali hii hadhi ya hili jukwaa limeshuka mno ujinga ni mwingi mno wachangiaji nao wapuuzi ni wachache mno wanaoujua mpira....
 
Mpira unachezwa uwanjani, wewe unaleta mambo yako ya kishirikina.

Inasikitisha kua na watu wa aina hii Azam huyu huyu alimfunga Yanga na akasababisha beki wa Yanga kupata kadi nyekundu,Je hao waganga wanaomsaidia Azam kushinda na kumdhibiti Simba wanaoletwa na Yanga waliamua kuisaliti Yanga na kua upande wa Azam?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…