Pre GE2025 Viongozi wapya wa Kanda ya Nyasa Waanza kazi rasmi

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Erythrocyte

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2012
Posts
128,308
Reaction score
245,426
Taarifa ikufikie popote ulipo kwamba viongozi wapya waliochaguliwa hivi karibuni Kanda ya Nyasa, Wameanza Kazi Rasmi leo.

Wamefika kwenye ofisi za Kanda ya Nyasa na kuanza kazi mara moja, Vigogo hao wazito wameongozwa na Mwenyekiti wao Joseph Mbilinyi, yumo pia Makamu Mwenyekiti Frank Mwakajoka na kupokelewa na Mwenyeji wao Katibu wa Kanda hiyo Gwamaka Mbughi.

PIA SOMA:

- Kuelekea 2025 - Joseph Mbilinyi (Sugu) ashinda uchaguzi Kanda ya Nyasa, amgaragaza Mchungaji Msigwa

- Kuelekea 2025 - Mchungaji Msigwa atangaza kukata rufaa kupinga Ushindi wa Joseph Mbilinyi (Sugu) Kanda ya Nyasa

 
Uongozi wa wanaume, mwanamke yupo mmoja Tena msindikizaji
 
kwamba viongozi ndio hao, wamejibana kwenye kaofisi na kameza kadogooo

halafu huyo jamaa anataka kutuambia kwamba mwenyekiti wa kanda hana computer sio, yeye pekee ndio anayo dah
 
Sugu ndio brain ya Chadema kanda yote ya Nyasa. Uko ni kuchanganyikiwa
 
kwamba viongozi ndio hao, wamejibana kwenye kaofisi na kameza kadogooo

halafu huyo jamaa anataka kutuambia kwamba mwenyekiti wa kanda hana computer sio, yeye pekee ndio anayo dah
Hatutakujulisha kila Jambo, tumekupa Dondoo tu
 
Mchungaji Msigwa kakata Rufaa lakini viongozi wataendelea πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Umefurahi tunakujua upo timu sugu!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…