Viongozi wawili wa upinzani, mahasimu wakubwa wa rais Yoweri Museveni wameachiwa huru

Viongozi wawili wa upinzani, mahasimu wakubwa wa rais Yoweri Museveni wameachiwa huru

Mapengo 17

R I P
Joined
Mar 28, 2014
Posts
1,229
Reaction score
610
Viongozi wawili wa upinzani, mahasimu wakubwa wa rais Yoweri Museveni katika uchaguzi ujao wa rais wameachiwa huru baada ya kukamatwa kwa saa kadhaa na polisi, kwa madai ya kutaka kuitisha kampeni za uchaguzi bila ya ruhusa.

Waziri Mkuu wa zamani Amama Mbabazi na Kizza Besigye mojawapo ya vigogo wa chama cha upinzani FDC walikamatwa jana walipokuwa wanajiandaa kushiriki katika mikutano ya kisiasa.

Viongozi hao wawili wametia saini waraka kwa hivyo wameachiwa huru bila ya masharti. Polisi nchini humo imeonya haitovumilia mikutano ya kisiasa itakayoitishwa bila ya ruhusa.

Wahusika wanabidi kutuma ufafanuzi wa mikutano kwa polisi siku tatu kabla ya kuitishwa.
 
Back
Top Bottom