Filipo Lubua
JF-Expert Member
- Nov 18, 2011
- 339
- 578
Wadau,
Tumeshuhudia wanafunzi wengi wakifeli darasa la saba wanavyosota mitaani bila mahali pa kwenda, hasa wazazi wao wasipokuwa na uwezo wa kuwapeleka shule binafsi.
Kwa sababu hii pia, bila shaka tumekutana na watu walioko katika kada mbalimbali wakituhumiwa kuwa na majina ya kununua baada ya kufeli mtihani wa darasa la saba. Miongoni mwa viongozi wa kitaifa waliokutana na kashfa hizi ni Naibu Waziri wa Elimu Philip Mulugo, Naibu Katibu Mkuu CUF Julius Mtatiro, na Naibu Katibu Mkuu CCM Mwigulu Nchemba.
Nikiachana na Philip Mulugo ambaye tetesi zinasema alibadili jina baada ya kumaliza kidato cha nne, Mwigulu Nchemba anasemekana kuwa jina lake halisi ni Lameck Mkumbo Madelu, wakati Julius Mtatiro akisemekana kuwa jina lake halisi ni Sunday Charles.
Mimi sihitaji kuthibitisha kama kweli viongozi hawa walinunua majina au waliiba majina kama walivyotuhumiwa. Ninachohitaji kusema hapa ni jinsi mfumo wetu wa Elimu ya Msingi unavyowanyima wanafunzi wanaofeli haki ya kuendelea na masomo. Mwanafunzi anapofeli mtihani wa Darasa la Saba (au anapofaulu lakini kwa uhaba wa shule akakosa nafasi ya kujiunga kidato cha kwanza) anakuwa hana pa kwenda, hasa wazazi wake wasipokuwa na uwezo wa kumpeleka shule binafsi. Wengi wao hutafuta njia mbadala za kuendelea na masomo, hasa kwa kununua majina ya wanafunzi walioacha shule wakiwa darasa la tano au sita. Wanaponunua majina haya, hufanya mtihani huo kwa majina feki, na wanapofaulu, hulazimika kuendelea nayo. Hili husababisha wengi kukutwa na kashfa hizi za akina Mtatiro na Mwigulu. Wengi tunawafahamu watu wa namna hiyo, hasa maeneo ya vijijini, hata mimi nimemaliza na watu wa namna hiyo.
Hoja yangu ni kuwa, kwa nini mfumo wa elimu yetu usitafutiwe njia mbadala ya kuwakaririsha wanafunzi wanaofeli darasa la saba, kama ilivyo kwa Kidato cha Pili, Nne na Sita? Kwanini wanafunzi wanaofeli darasa la saba wasipewe fursa ya kurudia mtihani, kama ilivyo kwa mitihani mingine ya ngazi zinazofuata?
Nawasilisha kwa nia njema kabisa. Nawaomba Watanzania tutoe maoni, na si kusigana kwa itikadi za kivyama au kisiasa.