Viongozi wetu jihadharini na msivilee Vikundi Vya Machawa Ndani ya Vyombo vya Usalama nchini wanawaharibia badala ya kujenga na ipo siku watawageuka

Viongozi wetu jihadharini na msivilee Vikundi Vya Machawa Ndani ya Vyombo vya Usalama nchini wanawaharibia badala ya kujenga na ipo siku watawageuka

covid 19

JF-Expert Member
Joined
May 9, 2014
Posts
6,967
Reaction score
17,452
Nikiwa mwanachama wa kawaida wa CCM, najivunia sana historia na harakati za chama chetu tangu enzi za uhuru. Hata hivyo, naona kuna mambo yasiyo sawa yanayotokea hivi sasa, ambayo yanatia hofu kubwa kwa usalama wa raia nchini.

Tukio la hivi karibuni la kuuawa kwa Mzee Kibao na mfululizo wa matukio ya utekaji na mateso, yanayolenga wanachama wa CHADEMA pekee, yanatoa taswira mbaya.

Hii inahatarisha imani ya wananchi na wahisani kuhusu usalama wa raia wetu. Ingawa siwezi kusema wazi ni chombo gani kinaendesha haya matukio, nahisi kuna kikundi cha machawa kilichopo ndani ya vyombo vya usalama ambacho kinachukua hatua hizi kwa minajili ya kutetea CCM na viongozi wa nchi.

Swali langu ni, hivi kweli CHADEMA ina nguvu ya kuogofya kiasi cha vikundi hivyo kuachiwa kufanya watakalo sababu tu wapo kwenye vyombo vya usalama? Naogopa kusema kuwa hii si kweli. Kuna jambo ambalo halipo sawa.

Hofu yangu ni kuwa vikundi hivi vikishapata nguvu, havitatosheka. Mwisho wa siku, vitaanza kuwatafuta hata viongozi wa CCM wenye mitazamo tofauti na wale walio madarakani. Hii inaweza kuleta taharuki kubwa, na kufanya kila mtu kuishi kwa hofu—wananchi wa kawaida, wapinzani, na hata wanachama wa CCM.

Ninaungana na Rais wetu mpendwa, Mama Samia, katika kuomba kumalizwa kwa makundi haya. Nguvu zielekezwe kwenye majukwaa ya kisiasa, si kwenye kuondoa uhai wa Watanzania wenzetu. Vyama vya upinzani, kwa sasa, havina nguvu ya kuweza kuiyumbisha nchi, lakini baadhi ya machawa walioko kwenye vyombo vya dola wanatumia nguvu kubwa kuaminisha kuwa CHADEMA ni tishio.

Soma Pia: Ally Mohamed Kibao auawa na mwili kutelekezwa Ununio ukiwa umeharibika sana

Kama taifa, hatutaki kuona Watanzania wakiishi kwa hofu. Tunahitaji amani, siyo uhasama.

Poleni sana wafiwa, na poleni sana wanachama wa CHADEMA.
 
Back
Top Bottom