Mkuu kidogo ungenikata mbavu zangu. Naona hii itakuwa kali ya kufungia mwezi. Ni kweli kwa mazingira ya Osterbay kuna ulazima wa kuweka Tangazo kwa kiingereza sababu wapo wageni wengi. Lakini siamini kwamba alikosekana kabisa mtu wa kuipitia hiyo barua kabla ya kubandikwa. Hii ndivyo tunavyotaka tuonekane machoni kwa wageni!!.
Huyu naye!! Ila na sisi wa-TZ kwa kushobokea Kiingereza bwana! Hapo ukute ameamua kuliweka kimya kimya bila kushirikisha wengine ili watu pale Kitaa wamwone yuko juu, yaani Mwenyekiti wa mtaa wetu hapa Oyster bay anashuka Kiinglishi ni mwisho wa maneno!!!
Kuna haja ya watanzania kukubaliana namna ya kuwapata viongozi wenye uelewa lakini pia wenye kufahamu lugha gani watumie kwa njia ya mawasiliano hembu angalieni viongozi wenu wa CCm wanavyowasiliana kwa lugha ya kingereza
Turudi nyuma kidogo, hivi tukiambiwa baadhi yetu humu JF tuirekebishe hiyo barua, ni wangapi watathubutu? Mushi amethubutu, ameweza na anasonga mbele. Ujumbe umefika kwa walengwa.
Si bora ya huyu aingie bungeni , umewahi ona mbuge Lusinde au Majimarefu wanapokuwa kwenye kamati za bunge halafu kukawa na bahati mbaya ya kukutana na Mzungu??? utawaona wanajisogeza nyuma taaraaatiiiibu ... mpaka wapate usawa wa mwishoooo kabisa na kuwaachia wenzao wanaopandisha slang wakae mbele hapo ndipo nyoyo zao hupata amani