VIONGOZI WETU SIMBA,YANGA,NA HATMA YA SOKA LETU,

nkungu mwere

JF-Expert Member
Joined
Sep 6, 2018
Posts
258
Reaction score
336
Kwanza niseme wazi mimi ni mpenzi wa yanga,lkn hilo lisitafsiriwe kuwe mawazo yangu ni ya kishabiki,hivyo mjadala ujikite kwenye hoja na si ushabiki,niwakumbushe kuwa SIMBA SC ndio mabingwa wa TZ 2018/19 na 2019/20,hivyo kimahesabu tunaweza kusema kiwango cha simba kinapanda siku hadi siku,kwa sababu mwaka jana simba ilitolewa mapema klabu bingwa afrika,lkn mwaka huu pamoja na kutwaa ubingwa wa nchi kwa mara ya pili lkn imeweza kufika ROBO FAINALI AFRIKA,kwa maana hiyo kitaalamu tunasema kikosi cha simba kimekomaa na kimekuwa bora kuliko mwaka jana,sasa MAAJABU ni kuwa badala ya kukifanyia marekebisho kidogo penye mapungufu viongozi wameona bora wavunje kikosi kilichofika robo fainali na wasajili upyaa,hii si sahihi,kwa mashabiki wanaona ni sahihi,lkn wajue kusajili nusu ya kikosi ni hatari maana lazima kikosi kipya kianze upya,kwa lugha ya kawaida huwezi kupanga kikosi cha simba ukathubutu kuwaacha nje wabrazili wa 3,ukamwacha msudani,ukamwacha kagere,ukamwacha chama,ukamwacha kahata alafu utegemee kueleweka kwa mashabiki,jambo hilo (la kusajili nusu ya kikosi)linawezekana iwapo litafanywa na timu kama yanga ambayo inajulikana kikosi chake kimeshuka kiwango kiasi cha kupoteza ubingwa mara mbili,japo nayo yanga haikustahili kusajili baadhi ya wachezaji kutokana na historia yao(hili ntalizungumzia kesho)
 
Makala yako INA kitu ndani yake, ila imekata ghafla. Bila shaka mleta Uzi utarudi tena kuuendeleza Uzi huu, ili kukidhi matarajio ya msomaji. Kimsingi Uzi wako umeuanza vizuri sana na maudhui yake ni ya kujenga, msingi wa mjadala wako ni suala LA usajili mpya na madhara yake kwa timu husika.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…