Aaron Tebeka
Member
- Aug 1, 2022
- 6
- 6
Nipende Kutanguliza Shukrani zangu za Dhati kwa Jamii Forums kutufanya Kuyafikisha Yaliyokuwa Vichwani Mwetu Kwa Jamii Hii kwa Manufaa Ya Taifa Letu. Katika Kutangulia kwa Makala Hii nianze kwa Kuelezea kidogo kuhusu kipaji.
Kipaji ni Uwezo Ambao Anapewa Mtu katika kulifanya Jambo fulani kwa ufanisi wa hali ya juu na Mungu mwenyewe.
Kwahiyo tunaweza kusema Mtu akiumbwa lazima anapewa Mtaji Wa kuyafanya Maisha yake kuwa bora ambao ndiyo Kipaji Chenyewe.
Mtu Mwenye kipaji katika jambo Fulani, huwa Analimudu kwa usahihi Wake hivyo kuvuta Mafanikio Makubwa Sana Katika Shughuli hiyo.Tuchukulie Mfano, Mpira Wa Miguu, Lionel Messi Amekuwa akionekana bora zaidi katika mpira Kwa sababu ya Kuzaliwa na kipaji hiki Mguuni pake, Hali ambayo inampatia Mafanikio Makubwa Sasa hivi katika Soka.
Mtu mwenye kipaji Anahitaji juhudi za kawaida sana ili Kulifanya Jambo fulani.
Kwa bahati njema hakuna Mtu Ambaye anazaliwa bila kipaji, hapana! Isipokuwa Ugumu huanzia kwenye kukigundua kipaji hiki.Kwahiyo mwisho Wa siku tunajikuta Tunalazimisha Maisha Tu na Mwisho kufeli.
Kipaji Pekee ndicho huwaweka watu katika eneo Sahihi la Kutafutia Mafanikio na Wala Si Interview au Uchaguzi tuufanyao kila siku.
Mpaka Hapa ndipo Tunaona
Nini Sababu Ya Tanzania kuwa Nyuma Kimaendeleo?
Sababu kubwa ya Suali hili ni;
1/Uwekezaji Mdogo Unaofanywa na Serikali Kwenye Vipaji Na
2/Imani haba/Au vipaumbele Vya Wazazi au walezi Kwa Wanao.
Kuhusu Uwekezaji Wa Serikali,
Tunapoongelea UWEKEZAJI hapa tunaangalia Jitihada za Serikali au kuhamasisha Vipaji kukuzwa kwa Raia wake.
Tanzania Vipaji vimepuuzwa na ndio maana kuna Ufinyu Mkubwa Wa Shule za Vipaji Vya aina zote, Pamoja na Mashindano Makubwa ya Vipaji yenye Faida.
Madhara yake Watu wote wamekuwa wakijikuta wanalazimika kusoma mambo ambayo hawakupangiwa na Mungu wala wao hawayataki wawapo shuleni na Mwisho wanakuja kukumbana na uhaba Wa Ajira Mtaani.
Hapa kuna Haja ya kutengwa Fedha Za kutosha ili kulibadili hili.
KUHUSU VIPAUMBELE VYA WAZAZI/WALEZI.
Si suala la kushangaza kabisa kumkuta Mzazi/mlezi akimlazimisha mwanae Akasomee Udaktari na Si mziki/mpira au sanaa nyingine kama mwanae alivyotaka.
Hii ni kutokana na Kipaumbele cha wazazi Wengi kuwa katika Elimu tena ile ya What is history Na Digestion system.
Mtoto Kusoma Ni vyema na iwe lazima lakini Asome katika Njia ya kukuza kipaji Chake,Tafakari kama mtoto Akisoma katika Academy ya mpira kuna Ubaya gani?Unagundua ni njia nzuri sana Ya kumwandaa Mwanao kimaisha
FAIDA ZA KUVIPA KIPAUMBELE VIPAJI
1/Inapunguza tatizo la Ajira kwa kufanya watu wajikite kwenye Vitu wanavyoweza na si kurundikana kusubiri Ajira za Udaktari nakadhalika.
2/Inakuza Maendeleo katika Sekta zote za Kiuchumi kwa sababu kazi zitakuwa zinafanywa kwa Weredi si kibahatisha.
MADHARA YA KUTOVIPA VIPAJI KIPAUMBELE
1/Kuongeza tatizo la upungufu wa Ajira kwani watu watarundikana kwenye Fani moja kama ilivyo nchini,Udaktari.
2/Kupungua kwa ufanisi wa kazi kwa sababu ya Watu kuwa na ujuzi haba katika Shughuli Fulani
3/Kuongeza Suala la RUSHWA kwa kasi kubwa kwa sababu ya ufinyu wa Ajira.
Nini kifanyike?
Njia ya kutatua Tatizo hili ni kushirikiana kwa serikali na Wazazi, kwanza, kuwekeza sana katika kukuza vipaji na Pili Wazazi kuhakikisha kwamba mpaka mtoto anafikia Umri wa kubarehe anajulikana ana kipaji gani na kukitengenezea mazingira ya Kukikuza.
Kuiga si Ujinga bali kuiba, Wenzetu wazungu wamewekeza sana katika vipaji na Ndio maana wameendelea kutushinda sisi kiuchumi,Ukiangalia katika mipira, Uigizaji, Muziki nakadhalika kuna utajiri Mkubwa sana uko huko Na ni kwa sababu Ya kuvilea vipaji.
Mtoto Anapozaliwa, Anapaswa aletewe vitu vingi vya kuchezea na si mondori pekee,Iwepo mipira, redio, vinanda na mambo mengi ambayo yanahusika katika taaluma fulani na kile ambacho mtoto atapendelea kutumia sana mara nyingi ndo kipaji au uwezo ambao Anao na kama akilelewa hivyo atafanikiwa.
Kama tutaendelea kulazimisha hakuna Mabadiliko tutakayopata kiuchumi ,Zaidi ya kupanda na Kushuka tu.
Hapa kuna haja pia ya Serikali kuacha kuangalia Upande Mmoja tu wa Elimu kama kuhimiza Usomaji Wa Sayansi Ambao kwa kiasi kikubwa umeathiri Vichwa Vya taifa zima.
Sasa hivi kila Mzazi au mlezi atajisikia Amani kama atasikia Mwanae anasoma Sayansi kwa Sababu Eti Masomo hayo ndiyo yenye Ajira! Hapa tunalipoteza Taifa la kesho kwa kiasi kikubwa
Kwa Jinsi hii tunaandaa Taifa kubwa la vijana wasio na Ajira na la wale Wavivu Wanaoketi kijiweni kutwa na Mwisho wa Siku kiwa Wezi na vibaka
Jicho lionalo kesho Linahitajika Sana Hapa! Ukifuatilia kwa Umakini Utagundua kuwa Vipaji Vimewainua Wengi Sana na Hatimaye nao Wanawainua Wenzao.
Angalia Mfano, Katika Mpira hapa nchini,Mbwana Samatta anafanya vizuri sana kimataifa lakini ukitazama kiundani unagundua Umri Unakuja kuwa kikwazo kwa ndoto Zake Ilhali hajazitimiza kama vile Anavyotaka na hili ni kwa sababu ya mwitikio mdogo wa Wazazi/ Walezi katika vipaji na pia kipaumbele cha Serikali.
Lakini kwa upande Mwingine,Kama utakuwa Mfuatiliaji Mzuri Utagundua kuwa Tanzania ni nchi ambayo Imebarikiwa Vijana Wengi Wenye Vipaji ila Wengi wao wako mtaani tu hawana hili wala lile,Wamekosa Msaada,,Sasa Je hawa ndo wale Vijana tunaowaandaa kuwa Taifa la Kesho?Tujichunguze
V NIMALIZIE KWA KISEMA KWAMBA, Tunapoandaa Taifa la kesho ni lazima liwe Taifa kubwa lenye Mafanikio Kiuchumi na kwa kila Kitu, Na si Maskini, Wezi, Watoa Rushwa, Na vibaka. Kwahiyo hawa Vijana Wetu ambao Tunawaita, Taifa la Kesho, Lazima tuwafanye Wakubwa kwa kuwaweka kwenye Sekta Ambazo Zinawafaa. Na Njia Pekee ya Kuzijua Sekta hizi zinazowafaa Ni kwa kuangalia Vipaji Vyao tu Na si vinginevyo.
Asante Kusoma!Fikisha Ujumbe Huu Mbali Zaidi.
MUNGU IBARIKI TANZANIA

Upvote
1