The Sheriff
JF-Expert Member
- Oct 10, 2019
- 747
- 2,112
Baada ya kushinda uongozi ulioshikiliwa kwa karibu miongo sita na chama kimoja, hivi ni vipaumbele vitano vya Rais mpya wa Botswana, Duma Boko, kama alivyoahidi wakati wa kampeni na hata baada ya kushinda kiti hicho. Wananchi wa Botswana wanataraji kuona ahadi hizi zikitekelezwa kwa imani kuwa mabadiliko ya chama yanaweza kuwasogeza mbele kimaendeleo.
1. Kurekebisha hali ya uchumi
Rais Boko anakabiliwa na changamoto kubwa ya kifedha kwani uchumi wa nchi umeathiriwa na kuporomoka kwa bei za almasi, bidhaa ambayo kwa muda mrefu imekuwa msingi wa uchumi wa Botswana. Almasi za kutengenezwa zimeleta ushindani mkali kwa almasi asilia, na kusababisha kushuka kwa mapato ya nchi. Rais Boko na chama chake cha Umbrella for Democratic Change wameahidi kuongeza kasi ya ukuaji wa uchumi hadi kufikia zaidi ya asilimia 10, pamoja na kuunda ajira 500,000 katika miaka mitano ijayo. Pia ameahidi kuongeza pensheni ya wazee kutoka kiwango cha sasa cha pula 830 (Tsh. 163,000) hadi pula 1,800 (Tsh. 353,000), ili kuboresha maisha yao.
2. Kufikia makubaliano ya biashara na kampuni ya almasi ya De Beers
Rais Boko ameonyesha nia ya kujenga uhusiano mzuri na De Beers baada ya sintofahamu iliyokuwepo kwenye uongozi uliopita. Rais aliyemaliza muda wake, Mokgweetsi Masisi, alifikia makubaliano ambayo yangeipa Botswana asilimia 50 ya almasi inayotokana na ushirikiano wa Debswana katika kipindi cha miaka kumi ijayo, lakini mkataba huo haukusainiwa. Rais Boko anataka kuelewa changamoto zilizokuwepo na kutafuta suluhu inayowezekana kwa manufaa ya pande zote, lengo lake likiwa ni kuimarisha uchumi kupitia makubaliano hayo ya kibiashara.
3. Kuhakikisha vikosi vya usalama vinasimamiwa na kuongozwa ipasavyo
Kwa muda mrefu, Idara ya Usalama wa Ujasusi na Ulinzi (Directorate on Intelligence and Security Services) imekuwa na mgawanyiko wa uaminifu, huku baadhi ya maafisa wakimuunga mkono Rais mstaafu Ian Khama katika mgogoro wake na Rais Masisi. Migawanyiko hii imefanya baadhi ya maafisa kwenda kinyume na sheria na kushindwa kushirikiana na vyombo vingine vya usalama kama Idara ya Kuzuia Ufisadi na Uhalifu wa Kiuchumi. Rais Boko ana nia ya kuwaunganisha na kuhakikisha kuwa wanazingatia majukumu yao kisheria na wanatoa huduma kwa wananchi kwa haki.
4. Kupambana na ufisadi ambao umekuwa ukiongezeka
Utafiti uliofanywa na Afrobarometer mwaka 2022 unaonesha kuwa wananchi wanaamini rushwa imeongezeka, huku baadhi ya miradi mikubwa ya serikali ikihusishwa na ndugu wa viongozi. Pia kuna taarifa kuwa baadhi ya maafisa wa serikali walikuwa wakiharibu nyaraka zinazohusisha mikataba yenye ufisadi baada ya kuona kwamba chama tawala kinapoteza uchaguzi. Rais Boko anataka kurejesha imani ya wananchi kwa taasisi za umma kama mahakama na vyombo vya kupambana na ufisadi kwa kuhakikisha vinashughulikia kesi za ufisadi kwa haki na ufanisi.
5. Kuimarisha mahusiano na nchi jirani
Rais Boko ana mpango wa kuwapatia vibali vya muda vya kazi na makazi Wazimbabwe wanaoishi Botswana bila vibali ili waweze kufanya kazi zao kihalali. Botswana ina idadi kubwa ya wahamiaji kutoka Zimbabwe, ambao wanakimbia hali ngumu ya kiuchumi nyumbani kwao. Kukosekana kwa vibali kumesababisha baadhi yao kuishi kinyume na sheria na wakati mwingine kujihusisha na uhalifu. Rais Boko pia anataka kuimarisha biashara na Afrika Kusini baada ya Botswana kupunguza uagizaji wa mazao kutoka Afrika Kusini miaka mitatu iliyopita ili kuendeleza kilimo cha ndani. Hatua hii iliathiri upatikanaji wa baadhi ya mazao nchini na kusababisha malalamiko kutoka kwa wananchi. Rais Boko anaamini kuwa kuimarisha mahusiano na nchi jirani kutasaidia Botswana katika ukuaji wa uchumi na utulivu wa kijamii.
Je, Rais Boko atafanikiwa kushikilia imani ya watu wa Botswana au atatoa boko?