mkongo
Member
- Nov 21, 2009
- 19
- 9
Nimekuwa nikiangalia baadhi ya habari na imenisikitisha sana Uamuzi wa Gavana wa Tanzania kutumia fedha nyingi kukarabati/kujenga nyumba ya kuishi YEYE. Yaani kupewa tu nafasi hiyo anataka aishi nyumba ya kifahari. Je alikuwa wanaishi kwenye nyumba ya kifahari kabla ya kupewa cheo hicho? Ingekuwa fedha hizo zinatoka mifukoni mwake angejenga nyumba hiyo ya kifahari? Hakuna mtu asiyependa maendeleo lakini tuwe na huruma, hivi wewe GAVANA hujaishi maisha ya mtanzania ya kijijini? Huoni shida wanazopata wananchi wa kijijini? Na sio tu kijiji mijini pia kuna shida pia ambazo Serikali inasikilizia kutatua. Inaweza kuwa Benki Kuu labda haihusiki moja kwa moja na kutatua matatizo ya mwananchi basi Vipaumbele vya Benki kuu nini? Kujenga nyumba ya Gavana? (Jibu langu ni HAPANA lakini la Prof.Ndulu ni NDIYO). Waliomweka huyu Prof. Ndulu madarakani wanasemaje kuhusu suala hili? Tumekaa kimya tunawasubiri waseme
wanatakiwa kuwajibika kwetu kwa hiyo tunawasubiri. Tanzania ni nchi ya ajabu baadhi wa watu wachache (Viongozi) wenye madaraka na nguvu wameamua kujifanya wenyewe sio sehemu ya Matatizo ya Watanzania. Angalia
1.Tatizo la barabara mbovu (Wanajinunulia mashangigi). Mwananchi wa kawaida shauri yako
2.Uduni wa shule zetu (Wanasomesha watoto nje ya nchi). Mwananchi wa kawaida shauri yako
3.Uduni wa mahospitali na huduma za afya (Wanaenda nchi za nje kutibiwa) Mwananchi wa kawaida shauri yako
4.Umeme unakatikakatika (Wana majenereta au haukatwi sehemu wanazoishi). Mwananchi wa kawaida shauri yako
5.Orodha inaendelea
Ewe Kiongozi wa Tanzania ACHA UBINAFSI na yule aliye kijiji au anayepata hizo shida ni Mtanzania/binadamu kama wewe. Ulichaguliwa au kupewa hayo madaraka kumtatulia shida zake na sio shida zako. Ni hayo kwa leo wajameni.