Watu wanaendelea kutumia .com kama kawaida kwa sababu uhuru wa habari siyo mapenzi,hisani,kudra wala takwa la Rais wala taasisi yoyote ile bali ni takwa la kikatiba.Kuzuia matumizi ya .com Tanzania ni kuminya uhuru wa habari pamoja na uhuru wa kujieleza ambao ndiyo msingi wa katiba yetu.Sheria kandamizi kama hizi zinapaswa kupingwa hadi na mawe ambayo hata uhai hayana.
Suala la uhuru wa habari na haki za kujieleza ni haki yetu kikatiba.
Haki huwa haiombwi wala huwa haitolewi bure kama unavyodhania bwana mleta uzi bali haki huchukuliwa kwa nguvu na ndiyo maana watu wanaendelea kutumia .com bila wasiwasi wowote ule.
Rais na taasisi zozote zile hazina wajibu wala haki wala nguvu wala amri ya kuzuia au kuruhusu watu kutumia .com na pia hatuna haja wala wajibu wa kumuomba Rais wala taasisi yoyote ile iruhusu matumizi ya .com Tanzania bali ni haki yetu na mtu yoyote yule ikiwa ni pamoja na Rais au taasisi yoyote ile ikituzuia tuna wajibu kikatiba wa kuchukua haki hiyo kwa nguvu kwa sababu uhuru wa kujieleza ni haki ya msingi katika katiba yetu.
Rais na taasisi zozote zile zitake zisitake suala la kutumia .com Tanzania ni haki yetu kikatiba wala siyo mapenzi yao na wasipotaka tuna wajibu kikatiba wa kuwalazimisha.
Umeelewa mleta mada?