Vipi kuhusu katiba ya Kenya inasemaje endapo mgombea aliyeshinda urais hana viti vingi bungeni?

Vipi kuhusu katiba ya Kenya inasemaje endapo mgombea aliyeshinda urais hana viti vingi bungeni?

Nondoh

JF-Expert Member
Joined
Aug 26, 2016
Posts
298
Reaction score
478
Kwanza kabisa natoa pongezi zangu kwa majirani zangu wakenya kwa hatua nzuri ya kidemokrasia waliyofikia. Binafsi nampongeza Jaji aliyetoa maamuzi, Raila Odinga kwa kutumia mahakama kudai haki yake badala ya kupeleka watu barabarani, Uhuru Kenyatta na wakenya kwa ujumla kwa utulivu waliyouonyesha baada ya Kenyatta kutangazwa mshindi.

Pongezi kubwa zimwendee Uhuru Kenyatta kwa kuiishi demokrasia kwa vitendo, tofauti na viongozi wengine wa afrika ambao ni wanafiki wa demokrasia. Ameonyesha utu kwa kutouingilia mfumo wa mahakama na kuupa uhuru (kama jina lake) kutekeleza majukumu yake. Kuwa na katiba nzuri ni suala jingine na kuiishi katiba nzuri ni suala jingine lakini ameweza.

Turudi kwenye swali:

1. Je uchaguzi utarudiwa kwa ngazi ya urais tu au ngazi zote?

2. Je kama ni ngazi ya urais tu vip matokeo kwa ngazi zingine, yalikipa (majority) chama/muungano gani ushindi?

3. Endapo Odinga atashinda je ataweza kuunda serikali kama uchaguzi ngazi zingine hautarudiwa na kama uchaguzi uliopita upande wa Kenyatta walishinda viti vingi?

4. Je katiba ya sasa ya kenya inaruhusu serikali ya umoja wa kitaifa (coalition government)?
 
Uhuru Kenyatta anataka kubadilisha katiba ili kama kuna matatizo ktk teknolojia mahakama ya juu isiwe na mamlaka ya kufuta matokeo kwani Jubilee ina wabunge wengi

Sent from my TECNO-C5 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom