Iko hivi, Simba msimu uliopita walisajili jumla ya wachezaji 15 katika madirisha yote mawili , msimu ubao anza hadi sasa wamesajili wachezaji 13 ina maana ndani ya mwaka mmoja ndani ya Simba wameingia wachezaji jumla ya 27 na kuondoka wachezaji Kwa idadi hiyo hiyo! Kwa maana nyingine Simba imevunja uti wa mgongo wa timu na inajenga timu mpya, katika mazingira nayo, watahitaji muda wa kutosha , wa misimu kadhaa ili kuwa na timu imara, wakati nayo yanatokea kwa Simba,Yanga wao, wanatimu iliyo imara kwahiyo wanarekebisha pale palipo onyesha udhaifu ili kuwa na timu imara zaidi.Huwezi kuwa na timu imara kwa kusajili na kuacha wachezaji 27 ndani ya mwaka mmoja, huo ni utani, soka haliko hivyo!