Vipi mtu asiyejua kusoma na kuandika, aliyeishi miaka 1400 iliyopita akajua haya?

Katika Quran kuna baadhi ya sura zilishuka kutokana na mahitaji ya wakati husika
 
Wewe ndiyo WAKUJA sana. Kwa nini udhani mie nasoma Blog za Wazungu na siyo Wazungu wanasoma Blog yangu?
Mbona unajidharaulisha sana kwa Wazungu? Ni watu wa kawaida tu kama sisi. Usiwaogope kiasi hicho.

Sijasema kuna MALAIKA walikuja kutoka mbinguni ila kuna WATU. Na hilo limeandikwa hata kwenye hiyo Biblia yako agano la kale ila sikumbuki ni kitabu gani maana nina siku sisomi Biblia. Ila ukipata MJUZI wa Biblia basi atakuthibitishia maneno yangu na kukupa mistari.
Ila hapa tuweke mambo ya IMANI pembeni na tudeal na FACT. Nenda thread yangu ya #56 na angalia hizo film. Moja nimeweka juu hapo sasa hivi.

Sasa tuje kwenye Golden number vs Golden Ration na tujadili kwa FACT.





Kama unavyoona hapo juu: Equation ya kwanza ni GOLDEN RATION.
Ila naomba uniambie, 1.618.... ni nini hapo juu?
Au hiyo 1.618 ni BLOG ZA WAZUNGU?

Other Names:
The Golden Ratio is also sometimes called the golden section, golden mean, golden number,divine proportion, divine section and golden proportion.

 

Attachments

  • upload_2017-1-27_12-46-43.png
    15 KB · Views: 61
Fuatilia historia vzuri uone hvo vikundi vimeanzishwa Na nani na ni nani anaewapa ela ya kununua adi vifaru Ndo utaelewa vzur kabla hujaanza kuongea propaganda
Umeongelea vikundi kuanzishwa na nani na upatikanaji wa pesa kununua vifaru.
Vikundi vimeanzishwa na wapinzani ndani ya nchi either kupinga kutawaliwa katika sheria za kiislamu au kupinga kutawaliwa kidictator au kutaka nchi itawaliwe katika sheria za kiislamu.

Kwani Isis wanapewa silaha au pesa na nani? Isis inataka nchi zitawaliwe katika sheria kiislamu. Gaddafi na Saddam hawakutawala kwa sheria za kiislamu.

Swala kupewa silaha hatuwezi kuthibitisha jinsi wanavyozipata, ingawa kuna report kuwa Isis wanapewa support na Sunni countries.
Hivi nchi za kiislamu zinafanya vita kwa kuchochewa na nchi zingine? Kama ndiyo hivyo utakuwa na maana kwamba they can't think for themselves! Hawezi adua akaja kwako akawapa silaha ndugu zako alafu mkaanza kuuwana! Huwo ni ujinga. Tatizo ni siasa, dini na utajiri wa mafuta.
 
Hahaha ningekushauri ukasome number theory Na hata Euclid's elements of geometry lakini cdhani kama uko interested Na hesabu kabisa.Wewe endelea hvo hvo Mimi siitaji kumu elimisha mtu yoyote maana cyo wajibu wangu
 
Hapo iliyo tumika ni tafsiri ya kiswahili ambacho ata mwanafunzi wa darasa la sita anaelewa. Hamna ubulisheka hapo! Kama unayaongeza yako katika Quran, wewe endelea. Quran imekamilika kama inavyodai kwahiyo kama muislamu ongeza maneno at your own risk!

Unless kiswahili kinakusumbua basi hutoelewa, lakini hapo ni very clear katika.....Al-Kahf 18:86. Hata alipo fika machwea-jua aliliona linatua katika checmchem yenye matope meusi. Na hapo akawakuta watu. Tukasema: Ewe Dhul-Qarnaini! Ama uwaadhibu au watwae kwa wema.

Kwa kusisitiza Qur'an inaonyesha "...jua aliliona linatua katika checmchem yenye matope meusi."

Kama hutaki kubali sayansi iliyo andikwa hapo it's up to you. Kubali kutokubaliana na tusonge mbele, hatuwezi rudia au kukosoa maneno ya Allah. Allah ndiye anajua yote.
 
Sometimes jifunze tu kukubali ulichemka.

Yaani 1.618 unataka kuiita ni Ratio na siyo Number?

Anyway, wote tunaongelea jambo hilohilo. Ni kama Ice, Water and Vapour.... it's just H2O.
Wewe unasema KESHO na mie nasema Jumamosi huku leo ni Ijumaa.

Kwa taarifa yako hizi ni Fizikia zaidi kuzidi Hesabu. Inawezekana kweli wewe ni Mkali wa Hesabu ila unapobishana na Wahandisi basi sisi tunadeal zaidi na uhalisia na siyo Namba Hewa.

Kasome kitu kinaitwa Theory of Elasticity and Plasticity ndiyo utajua ninasema nini. Unacheza na namba katika vitu halisia. Tamu sana.

Nyie watu wa kumeza namba endeleeni maana ukiulizwa ina aply wapi kwenye maisha unabaki unaKODOA.
Nikutakie weekend njema.

Hahaha ningekushauri ukasome number theory Na hata Euclid's elements of geometry lakini cdhani kama uko interested Na hesabu kabisa.Wewe endelea hvo hvo Mimi siitaji kumu elimisha mtu yoyote maana cyo wajibu wangu
 
Uislam ulipita katika kipindi cha vita,hizo aya za mwanzo zilikuja ktk kipindi hali nishwari,na hizo nyingine zilishuka wakati wa mapambano.Au ulitaka ktk Uwanja wa mapambana Mohammad aambiwe " wakikukata mkono wa kulia wape na wakushoto waumalizie?"
 

Sasa nimeamini kabisa kuwa "Uislam" na "Waislam" ni wanafiki sana. Kama Quran yenu inawafundisha kuwa wana wa Israili walivushwa baharini na Mungu na tena inasema "hapana Mungu ila yule waliyemuamini wana wa Israili", sasa mbona ninyi Waislamu mnawapiga vita wana wa Israili?

Wanafiki wakubwa, mnajishuhudia wenyewe kwa mafundisho yenu.
 
Na wewe unaiga idiology za watanzania au waarabu? Watanzania ni wenye amani na nchi zote za kiislamu ni vita na terrorism. Bahati yako uko Tanzania! Nenda Libya uone terrorist watakufanya nini?
Nchi za kiarabu zenye via no Syria,Iraq na Lybia tuu,sio zote!
 
Hahaha hesabu ni pure elegance mkuu na Wewe cjui unasoma uhandisi gani ambao unakufundisha kuponde namba.Na Ndo maana tz waandisi hatuoni kazi mnazofanya kama ndo hvo mnafundishwa kuwa hesabu haina maana cdhani kama mtakuja tengeneza hata calculator
 
Hahaha eti hesabu haina application wewe unadhani kinachokupa privacy kwenye mtandao ni nini uhandisi au?? unadhani kinachofanya serekali isiweze ku crack password yako ni nini elasticity au ? Kuna vitu usiongee kabisa unaonekana waajabu mhandisi aoni umuhimi wa hesabu kweli ulienda chuo bure
 
Nashindwa kujua nikudharau au nikuache tu uendelee kuamini ndoto zako. Kwa taarifa yako mie sijasoma Chuo Kikuu chochote Tanzania. Hao Wazungu unaowaogopa nimewafundisha sana tu ili wapasi mitihani.

Turudi njiani: Kuna tofauti kidogo kati ya Maths na Apllied Maths kama kwenye IT, Physics, Civil Engineering nk. Mfano mdogo ni formula ya q= mc(delta)T ambayo tunaambiwa heat energy linategemea uzito, uwezo wake wa kupitisha joto na tofauti kati ya joto la mwanzo na la mwisho. Ila Mpemba Effect ina prove sivyo. Haya sasa hizo namba zako ziko wapi? Ndiyo tofauti ya Mhandisi na Mwana mahesabu. Mhandisi anatumia hesabu kumsaidia ila hazitegemei hesabu peke yake. Kuna vitu inabidi aviweke sawa akiwa Lab kwani hesabu zinagoma kuleta jibu sahihi. Ndiyo maana Engineering ina Coefficient nyingi sana.

Huu ni ujumbe wangu wa mwisho kukujibu. Kama utakuwa hujanielewa basi wewe umeshinda. Nakaribisha majadiliano ya kisayansi au kimahesabu zaidi na siyo malumbano. Nimeshafika home... ngoja niweke simu pembeni nifurahi na familia. Have nice day.


 

Sehemu uliyoongelea kuhusu pure Na applied math hapo Ndo naweza kubaliana Na ww Na jibu la kwanin hyo formula unavyodai inashindwa nabdi nifuatilie hyo kitu maana Mimi sijawahi maindisha phyzikia sana.Ila Pia unatakiwa tambua kuwa pure mathematics inatumika sana tu mfano prime number theorem IPO kazini hata humu jf.All in all hesabu ni fundamental mtaendelea Fanya engineering ila lazma mrudi kwa baba yenu hesabu mpate uelewa
 
That is what I thought about you. Do your homework to know much about Fizikia na ndiyo uje ujadiliane na Wahandisi.
Hii dunia kama hujui Fizikia, Chemistry na Hesabu basi usibishane na watu kama GT. Dunia hii imeumbwa na Fizikia pamoja na Chemistry. Hesabu zimekuja kufuata baadaye sana. Kama Algebra ambazo ndiyo msingi wa Algorythm zinazotumika hapa kwenye Computer au programing ni vitu vilivyogunduliwa mu-Iran Muhammad Al-Khwarizmi miaka kadhaa baada ya Yesu.

Unaonekana umri wako bado mdogo au umesoma Old School sana. Vitu vingi bado huvijui. Fizikia na hesabu vinaenda pamoja. Jitahidi uperuzi Fizikia ndiyo utajua jinsi Hesabu zinavyopewa Limitation kwenye mambo mengi. Good luck.
 
 
Quran 27:

1. T'aa Siin. (T'.S.), Hizi ni Aya za Qur'ani na Kitabu kinacho bainisha;
2. Uwongofu na bishara kwa Waumini,
3. Ambao wanashika Sala, na wanatoa Zaka, na Akhera wana yakini nayo.
4. Kwa hakika wale wasio iamini Akhera tumewapambia vitendo vyao, kwa hivyo wanatangatanga ovyo.
5. Hao ndio watapata adhabu mbaya kabisa, na hao katika Akhera ndio watapata khasara zaidi.


60. AU NANI yule aliye ziumba mbingu na ardhi, na akakuteremshieni maji kutoka mbinguni, na kwa hayo tukaziotesha bustani zenye kupendeza? Nyinyi hamna uwezo wa kuiotesha miti yake. Je! Yupo mungu pamoja na Mwenyezi Mungu? Bali hao ni watu walio potoka.
61. Au nani yule aliye ifanya ardhi mahali pa kutua, na akajaalia ndani yake mito, na akaweka milima? Na akaweka baina ya bahari mbili kiziwizi? Je! Yupo mungu pamoja na Mwenyezi Mungu? Bali wengi wao hawajui.
62. Au nani yule anaye mjibu mwenye shida pale anapo mwomba, na akaiondoa dhiki, na akakufanyeni warithi wa ardhi? Je! Yupo mungu pamoja na Mwenyezi Mungu? Ni machache mnayo yazingatia.
63. Au nani yule anaye kuongoeni katika giza la bara na bahari, na akazipeleka pepo kuleta bishara kabla ya rehema zake? Je! Yupo mungu pamoja na Mwenyezi Mungu? Ametukuka Mwenyezi Mungu juu ya wanao washirikisha naye.
64. Au nani anaye uanzisha uumbaji, kisha akaurejesha? Na nani anaye kuruzukuni kutoka mbinguni na kwenye ardhi? Je! Yupo mungu pamoja na Mwenyezi Mungu? Sema: Leteni hoja zenu kama nyinyi ni wasema kweli.
65. Sema: Hapana katika mbingu na ardhi ajuaye ya ghaibu isipo kuwa Mwenyezi Mungu. Wala wao hawajui lini watafufuliwa.
66. Kwani huo ujuzi wao umefikilia kuijua Akhera? Bali wao wamo katika shaka nayo tu, bali wao ni vipofu nayo.
67. Na wakasema walio kufuru: Tutapo kuwa mchanga, sisi na baba zetu, hivyo kweli tutakuja tolewa?
68. Haya haya tuliahidiwa sisi na baba zetu zamani. Hayakuwa haya ila ni hadithi za uwongo za watu wa kale.
69. Sema: Nendeni katika ardhi, na tazameni ulikuwaje mwisho wa wakosefu.

70. Wala usiwahuzunukie wala usiwe katika dhiki kwa sababu ya hila zao wanazo zifanya.
71. Na wanasema: Ahadi hii itatokea lini, ikiwa mnasema kweli?
72. Sema: Asaa ni karibu kukufikieni sehemu ya yale mnayo yahimiza.
73. Na hakika Mola wako Mlezi ni Mwenye fadhila kwa watu, lakini wengi wao hawashukuru.
74. Na hakika Mola wako Mlezi anayajua yanayo ficha vifua vyao na wanayo yatangaza.
75. Na hakuna siri katika mbingu na ardhi ila imo katika Kitabu kinacho bainisha.
76. Hakika Qur'ani hii inawasimulia Wana wa Israili mengi wanayo khitalifiana nayo.
77. Nayo hakika ni Uwongofu na Rehema kwa Waumini.
78. Hakika Mola wako Mlezi atawahukumu kwa hukumu yake, naye ni Mwenye nguvu Mjuzi.
79. Basi mtegemee Mweneyezi Mungu; hakika wewe uko juu ya Haki iliyo wazi.
80. Kwa hakika wewe huwezi kuwafanya maiti wasikie, wala kuwafanya viziwi wasikie wito, wanapo kwisha geuka kwenda zao.
81. Wala huwezi kuwaongoa vipofu waache upotovu wao. Huwezi kuwafanya wasikie isipo kuwa wenye kuziamini Ishara zetu; na hao ndio wat'iifu.
82. Na itapo waangukia kauli juu yao, tutawatolea mnyama katika ardhi atakaye wasemeza, ya kuwa watu walikuwa hawana na yakini na Ishara zetu.
83. Na Siku tutapo kusanya kutoka kila umma kundi katika wanao kadhibisha Ishara zetu, nao watagawanywa mafungu mafungu.
84. Hata watakapo fika, atasema (Mwenyezi Mungu): Je! Nyinyi si mlizikanusha Ishara zangu pasipo kuzijua vyema? Au mlikuwa mkifanya nini?
85. Na kauli itawaangukia juu yao kwa vile walivyo dhulumu. Basi hao hawatasema lolote.
86. Je! Hawaoni kwamba sisi tumeufanya usiku ili watulie, na mchana wa kuangaza. Hakika katika hayo zipo Ishara kwa watu wanao amini.
87. Na Siku litapo pulizwa baragumu, watahangaika waliomo mbinguni na katika ardhi, ila amtakaye Mwenyezi Mungu. Na wote watamfikia nao ni wanyonge.
88. Na unaiona milima unaidhunia imetulia; nayo inakwenda kama mwendo wa mawingu. Huo ndio ufundi wa Mwenyezi Mungu aliye tengeneza vilivyo kila kitu. Hakika Yeye anazo khabari za yote myatendayo.
89. Watakao kuja na mema, watapata bora kuliko hayo. Nao watasalimika na mahangaiko ya Siku hiyo.
90. Na watakao kuja na uovu, basi zitasunukishwa nyuso zao Motoni. Je! Kwani mnalipwa isipo kuwa mliyo kuwa mkiyatenda?
91. Ama mimi nimeamrishwa nimuabudu Mola Mlezi wa mji huu aliye ufanya ni mtakatifu; na ni vyake Yeye tu vitu vyote. Na nimeamrishwa niwe miongoni mwa Waislamu, wenye kunyenyekea.
92. Na niisome Qur'ani. Na mwenye kuongoka, basi ameongoka kwa faida ya nafsi yake; na aliye potea - basi sema: Hakika mimi ni miongoni mwa waonyaji.
93. Na sema: Alhamdu Lillahi, Sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu. Yeye atakuonyesheni Ishara zake, na mtazijua. Na Mola wako Mlezi si mwenye kughafilika na myatendayo.
 
Quran 69:

1. Tukio la haki.
2. Nini hilo Tukio la haki?
3. Na nini kitakujuulisha nini hilo Tukio la haki?
4. Thamudi na A'di waliukadhibisha Msiba unao situsha.
5. Basi Thamudi waliangamizwa kwa balaa kubwa mno.
6. Na ama A'di waliangamizwa kwa upepo mkali usio zuilika.
7. Alio wapelekea masiku saba, na siku nane, mfululizo bila ya kusita. Utaona watu wamepinduka kama kwamba ni magongo ya mitende yalio wazi ndani.
8. Basi je! Unamwona mmoja wao aliye baki?
9. Na Firauni na walio mtangulia, na miji iliyo pinduliwa chini juu, walileta khatia.
10. Wakamuasi Mtume wa Mola wao Mlezi, ndipo Yeye Mola akawakamata kwa mkamato ulio zidi nguvu.
11. Maji yalipo furika Sisi tulikupandisheni katika safina,
12. Ili tuyafanye hayo kuwa ni waadhi kwenu na kila sikio linalo sikia liyahifadhi.
13. Na litapo pulizwa barugumu mpulizo mmoja tu,
14. Na ardhi na milima ikaondolewa, na ikavunjwa kwa mvunjo mmoja,
15. Siku hiyo ndio Tukio litatukia.
16. Na mbingu zitapasuka, kwani siku hiyo zitakuwa dhaifu kabisa.
17. Na Malaika watakuwa pembezoni mwa mbingu; na wanane juu ya hawa watakuwa wamebeba Kiti cha Enzi cha Mola wako Mlezi.
18. Siku hiyo mtahudhurishwa - haitafichika siri yoyote yenu.
19. Basi ama atakaye pewa kitabu chake kwa mkono wake wa kulia, atasema: Haya someni kitabu changu!
20. Hakika nalijua ya kuwa nitapokea hisabu yangu.
21. Basi yeye atakuwa katika maisha ya kupendeza,
22. Katika Bustani ya juu,
23. Matunda yake yakaribu.
24. Waambiwe: Kuleni na mnywe kwa furaha kwa sababu ya mlivyo tanguliza katika siku zilizo pita.
25. Na ama atakaye pewa kitabu chake katika mkono wake wa kushoto, basi yeye atasema: Laiti nisingeli pewa kitabu changu!
26. Wala nisingeli jua nini hisabu yangu.
27. Laiti mauti ndiyo yangeli kuwa ya kunimaliza kabisa.
28. Mali yangu hayakunifaa kitu.
29. Madaraka yangu yamenipotea.
30. (Pasemwe): Mshikeni! Mtieni pingu!
31. Kisha mtupeni Motoni!
32. Tena mtatizeni katika mnyororo wenye urefu wa dhiraa sabiini!
33. Kwani huyo hakika alikuwa hamuamini Mwenyezi Mungu Mtukufu,
34. Wala hahimizi kulisha masikini.
35. Basi leo hapa hana jamaa wa kumwonea uchungu,
36. Wala hana chakula ila usaha wa watu wa Motoni.
37. Chakula hicho hawakili ila wakosefu.
38. Basi naapa kwa mnavyo viona,
39. Na msivyo viona,
40. Kwa hakika hii ni kauli iliyo letwa na Mjumbe mwenye hishima.
41. Wala si kauli ya mtunga mashairi. Ni machache sana mnayo yaamini.
42. Wala si kauli ya kuhani. Ni machache mnayo yakumbuka.
43. Ni uteremsho utokao kwa Mola Mlezi wa walimwengu wote.

44. Na lau kama angeli tuzulia baadhi ya maneno tu,
45. Bila ya shaka tungeli mshika kwa mkono wa kulia,
46. Kisha kwa hakika tungeli mkata mshipa mkubwa wa moyo!
47. Na hapana yeyote katika nyinyi ambaye angeli weza kutuzuia.
48. Kwa hakika hii ni mawaidha kwa wachamngu.
49. Na hakika Sisi bila ya shaka tunajua kwamba miongoni mwenu wapo wanao kadhibisha.
50. Na hakika bila ya shaka itakuwa ni majuto kwa wanao kataa.
51. Na hakika hii bila ya shaka ni haki ya yakini.
52. Basi litakase jina la Mola wako Mlezi Mtukufu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…