Nilinunua vocha ya shilingi 1000/= siku ya Jumatano juma lililopita,nilipojaribu kuingiza kwenye simu yangu nikaambiwa vocha hiyo haipo tayari kwa matumizi.Hii inakuaje maana niliwasiliana na watu wa VODA wakanambia vocha hiyo haijasajiliwa hivo niwe na subiri itakuwa tayari kwa matumizi ndani ya masaa 24ninachoshangaa mpaka leo ipo tu haijawa active>Sasa inakuaje bidhaa iingie sokoni halafu iwe bado haijasajiliwa? hivi ningekuwa nina shida ya muhimu na hela niliyokuwa nayo ni hiyo elfu moja tu hawaoni kama wangekuwa wameniweka katika wakati Mgumu?Kwa hili Vodacom sijawapenda kwa kweli sijajua nini tatizo au ndo tuanlipa ile kodi ile ya elfu moja kiaina?