Vipi Udom?

Muhwelo

Senior Member
Joined
Jan 16, 2013
Posts
136
Reaction score
32
Kwa sasa, Tanzania ina vyuo vikuu vingi; tunamshukuru Mungu kwa hilo. Baadhi ya majukumu makubwa ya vyuo vikuu ni kutoa elimu kwa wanafunzi na kufanya tafiti mbalimbali kwa maendeleo ya taifa zima. Taifa letu lina changamoto kibao zinazotakiwa kupatiwa ufumbuzi. Baadhi ya matatizo hayo ni kukithiri kwa ufisadi, uongozi mbovu, umaskini, maradhi, na mengineyo. Ndiyo maana kuna Maprofesa, Madaktari wa falsafa, nk. Chuo Kikuu cha Dodoma ni moja kati ya vyuo vikuu vikubwa na maarufu nchini, lakini wahadhiri wake wamejikita zaidi katika kufundisha tu kama wafanyavyo walimu wa shule za msingi na sekondari. Hiyo ndiyo kazi pekee ya Maprofesa na Madaktari wa falsafa hapo chuoni? Nauliza hivi kwa sababu matokeo ya tafiti nyingi zinazotangazwa kwenye vyombo vya habari zinatoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, SAUT, SUA na kwingineko. Vipi Udom? Sijawahi kusikia kutangazwa kwa matokeo ya tafiti kutoka Udom, wala wahadhiri kuikosoa serikali juu ya mwenendo wowote mbaya. Isipokuwa, nimewahi kusikia uongozi Udom ukiipongeza serikali. Je, wahadhiri wa Udom hawaoni dosari zilizomo nchini? Kuna mambo mengi ya kufanyia tafiti au kukosoa, kisiasa, kiuchumi na hata kijamii; au haya hawayaoni? Ama zile tetesi kuwa Udom ni chuo kikuu cha kisiasa, mara cha kata, ni za kweli? Kuna haja gani kuwa na chuo kikuu kisichokuwa na maslahi kwa taifa zima? Najua kuwa kuna tafiti za kitaaluma zifanywazo kimyakimya na wanafunzi wanaotafuta master's degree na PhD ambazo huanzia na kuishia maktaba, sawa. Maprofesa na Wanafalsafa, fanyeni tafiti zitakazotangazwa kitaifa ktk vyombo vya habari ili tuweze kutambua uwepo wa Udom kitaifa. Vile vile, fuatilieni mwenendo wa nchi yetu kiuchumi, kisiasa na kijamii. Sifa ya chuo kikuu haipatikani kwa kufundisha wanafunzi tu!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…