Johnny Sack
JF-Expert Member
- Jan 21, 2017
- 8,984
- 19,288
Wakuu habari,
Kama mnavyojua Rais Magufuli alileta kitu kilichoitwa Vitambulisho vya Machinga mwaka 2019
Vitambulisho hivi ambavyo vililipiwa 20,000 vilipelekea ushuru ambao machinga walikuwa wakilipa kwa Halmashauri kufutwa, na badala yake wangelipa hiyo 20k kila mwaka.
Sasa ni miaka 3 imepita na hivyo vitambulisho havijawahi kulipiwa tena, wala havifuatiliwi tena.
Kama halikuwa wazo zuri basi Serikali iendelee na utaratibu wa zamani wa machinga kulipia ushuru kwa halmashauri, maana wanafanya biashara bure huku serikali ikikosa fedha na kuweka kodi kubwa zinazoumiza wachache.