Vipi wakuu Same Boys Sec School

Lubaluka

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2009
Posts
496
Reaction score
44
Kwa wale waliosoma Same boy's Sec 1990 then kuwa mix skuli ( both gender ) around 1993...... tujikumbushe siku hizo.. Sisi ndio tuliokua kidato cha mwisho kilichoingia skuli hapo kwa jina la Same Boys ...

Mnakumbuka -- Masandare ( kijiji jirani na skuli )
Mwalimu Mziray aka 'kidudu mtu '
Je, picnic za mlima 'kwa koko' .... tunapanda na nyama ya mbuzi full kujiachia...
Na kuna Guest pale town maarufu sana kwa madent... jina limenitoka !!!

Gonjwa lisilo na tiba -- 'Njuka' yaani kidato cha kwanza

Du skendo ya kuwavamia Kirangare Girls Sec usiku wa manane walipokuja skuli kwetu kwa taaluma za maabara ( shule mpya haina maabara ) watoto wa mbwa ukame ulizidi... wakati wa likizo ndefu...

Mabweni ya mastaa wa skuli '' Nkuruma na Lumumba "

Mwalimu aka 'Kilio cha mti', 'Mshamba' real names nimesahau...
'
'Kutoboa' -- Kusoma usiku mzima bila kulala
Cheche - Wali mwanangu
Kuvua -- Kwenda jikoni na kuiba au chakula kabla ya muda halali.. kuchukua kwa magendo ????

Du, yule teacher wa chemistry -- wacha baba na ule mustachi wake...

so many more wana Same Boys Secondary --
 
Mimi nilisoma hapo kidato cha kwanza mwaka 1970!!
 
Hapo Dingswayo, hata sijazaliwa..... but then you have some history!!!!
 
Mimi nilikuwepo hapo enzi za Mhando, mkuu aiyebadili historia ya Same sec kwa uongozi shupavu. Alikaa muda mfupi, lakini matunda yake yalionekana. KILA LA KHERI MR.MHANDO POPOTE ULIPO
 
Wakuu.........

Nadhani kua thread nyingine ya Same inaexists na niliona mkuu amwanga alichangamsha kidogo mtoto yule

hebu chekicheki basi kama niko sahihi au la
 
Yap, Exaud Makyao let story... when ?? unakumbuka nini pale Ngusero.....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…