Vipimo Saba vya Ufanisi wa Kimkakati katika biashara

Vipimo Saba vya Ufanisi wa Kimkakati katika biashara

Masokotz

JF-Expert Member
Joined
Nov 26, 2018
Posts
3,713
Reaction score
6,121
Habari za wakati huu.Kama kawaida yangu huwa napenda kuleta mada na mijadala mbalimbali inayohusu biashara na ujasiriamali.Mijadala hii inalenga zaidi kupeana mbinu,ujuzi na uzoefu ambao utakuwezesha wewe mfanyabiashara mdogo uweze kufahamu kwamba kufanikiwa katika biashara sio swala la bahati bali ni swala ambalo linahitaji kujipanga na kufanya mambo kwa usahihi na uhakika.Leo ninawaletea vipimo saba vya kimakakati kwa ajili ya kufahamu iwapo biashara yako inaelekea katika njia sahihi.Vipimo hivi ingawa sio vya ukomo vitakupa mwangaza wa namna ya kuitazam biashara yako na kufahamu iwapo kuna uwezekano wa biashara yako kukua na kupiga hatua.Ukivitumia vipimo hivi unaweza kutambua uelekeo wa biashara yako na kufahamu matatizo na kuyarekebisha kabla hayajaleta madhara kwako.
  • Mkakati
Kipimo cha kwanza ca kimkakati ni MKAKATI wenyewe.Katika eneo hili unapaswa kufahamu iwapo biashara yako ina malengo ya kina na ya uhakika kuhusu uelekeo wako katika maeneo manne ya msingi ambayo ni masuala ya kifedha,uendeshaji,rasilimali watu na huduma kwa wateja.Ni muhimu ukajiuliza iwapo mipango na maamuzi unayofanyia yana faida au mdhara katika maeneo hayo manne ambayo ni moyo na msingi wa biashara yako.Kila unapofanya uamuzi ni lazima ufahamu faida za uamuzi huo kifedha,kiundeshaji,utendaji wa wafanyakazi na kukua kwa ubora wa huduma.Inapotokea kwamba jambo hili au uamuzi hauna faida ambayo inaoenekana katika ameneo hayo basi inapaswa usubiri mpaka utakapoona faida zake kwa kina.
  • Muundo
Kipimo cha pili ni muundo.Muundo unahusu zaidi nani anawajibika kwa nani.Katika uwajibikaji pia kunaswala la kila mtu kuyaelewa majukumu yake na kuwa na uwezo wa kuyatekeleza.Si hilo tu katika muunda ni lazima iwe wazi nafasi,uwezo na mchango wa kila nafasi iliyopo katika muundo wa usimamizi wa kampuni.Kila cheo na wadhifa lazima ueleweke katika muktadha wa faida zake kwa kwampuni.Hakuna sababu ya kuwa na mkurugenzi wa ICT iwapo kampuni ina computer moja ambayo mmiliki ni wewe.
  • Mfumo
Kipimo cha tatu ni Mfumo katika eneo hili inatazamwa zaidi upatikanaji wa taarifa na ufanyaji wa maamuzi.katika kampuni ni lazima ieleweke na iwe wazi ni nani anafanya maamuzi gani na wakati gani.Ni lazima pia iwe wazi je mfanya maamuzi anapata wapi taarifa za kumwezesha kufanya maamuzi.Kama mfumo wa upatikanji taarifa na ufanyaji maaumuzi hauko sawa unaweza ama kusababisha hasara au kupoteza fursa.
  • Mbinu za pamoja
Eneo hili mbinu za pmaoja ndio litatengeneza desturi ya kampuni yako.Je katika kampuni yake kila mfanyakazi anajihisi kuwa ni sehemu muhimu ya timu na kutambua nafasi yake na mchano wake katika kampuni?Je kila mfanyakazi anaamini kwamba anao uwezi na nafasi ya kuwa na mchango chanya katika kampuni au biashara yako?Ni muhimu sana kuhakikisha kwamba kila unalofanya linalenga katika kuhakikisha kwamba timu yako inakuwa na lengo moja la kuhakikisha kwamba biashara inakuwa na kupiga hatua mbele
  • Mtindo
Mtindo wa uongozi katika kampuni unaweza kuathiri utendaji wa kampuni.Kama biashara yako ina mtindo wa the Boss is always right basi usishangae kukawa na desture ya kupeana sifa za kijinga hata pale mtu anapokosea ila kama ana cheo basi hatakosolewa.Kama kampuni ina mtindo wa watu kufanya kazi kwa kujuana kufanya majungu na vijenmbe pamoja na fitna usishangae iwapo biashara yako itashindwa kupiga hatua.Mtindo wa usimamizi unaathiri sana maendeleo ya biashara yako.Ni lazima uwe na mtindo wa usimamizi ambao unaonesha uongozi,uwajibikaji na kujali wateja wa nje na wa ndani
  • Mfanyakazi
Kadiri biashra yako inavokua itafika hatua utahitaji kuajiri mfanyakazi.Katika hatua hii utahitaji kuhakikisha kwamba katika kuajiri wafanyakazi unaajiri watu wenye uwezo wa kutekeleza majukumu na wenye uwezo wa kukusaidia katika kufikia maelngo yako ya kibishara.Ni muhimu kuhikakikisha kwamba unaajiri aina ya wafanyakazi ambao watakuwa sehemu ya timu na ambao watakuwa "Compatible" na "team players" lazima wawe wanajituma wenyewe na wenye kuelewa malengo ya biashra yako na wawe tayari kushirikiana na wewe kuyafikia
  • Ujuzi
Katika eneo hili kipimo kinahusua utaalamu na ujuzi ulioko katika kampuni yako na namna ambavyo unatumika.Ni kosa kibiashara kuajiri mtu mwenye ujuzi wenye thamani kubwa na kutumia katika kazi zenye thamni ndogo.Ni muhimua sana kwa mfanyabiashara kuelewa aina za ujuzi ambao umo katika kampuni yako ikiwamo ujuzi wako binafsi na ujuzi wa watumishi wako.Ni lazima uwe tayari kuwapatia watumishi wako mafunzo na wewe mwenyewe kujipatia mafunzo ili kuhakikisha kwamba unakuwa na ujuzi sahihi wa kuweza kutoa huduma bora kwa wateja.

Karibu tujadili namna bora za kupiama ufanisi wako binafsi na ufanisi wa kampuni au biashara yako.Mbinu hii inaweza kutumika katika biashara ndogo au kubwa naitakupa mwanga wa iwapo biashara yako iko tayari kimkakati katika kuweza kukua na kufanikiwa katika ulimwengu wa kibiashara.Iwapo ungependa biashara au kampuni yako ifanyiwe Vipimo hivi vya ufanisi wa kimkakati tafadhali wasiliana nasi kwa Email masokotz@yahoo.com nasi tutashirikiana nawe pamoja na wataalamu wako katika kuhakikisha kwamba tunakupatia huduma bora na za uhakika.

Karibu tujadili mbinu nyingi za kupima ufanisi wa biashara yako.

Kuhusu SISI


Masoko Consulting ni Strategic Consulting Firm (Washauri waelekezi wa Kimkakati) ambao tunatumia mbinu za kisasa na utaalam wa kisasa katika kuwasaidia wateja wetu kutambua fursa na kuzitumia kwa ajili ya kukuza biashara zao na kukuza faida.Lengo letu ni kuwasaidi wafanyabiasha wadogo na wakati kubadilisha na kuboresha mfumo wa uendeshaji na usimamizi wa biashara zao ili ziendane na dunia ya kisasa kwa kuwawezesha kufikia zana za kisasa,utaalamu wa kisasa na teknolojia katika kuendesha biashara zao.

Sisi tunatoa huduma ya usajili wa Majina ya biashara,kampuni,leseni,TIN number NGOs,Taasisi za Kijamii,SACCOS,Taasisi za KIDINI,Taasisi za ELIMU,Viwanda,UWEKEZAJI na pia tunatoa ushauri juu ya namna bora ya kuendesha biashara yako.Unaweza kupata huduma hizo kwa gharama nafuu.Baadhi ya huduma hizo ni pamoja na:
  1. Kwanza tutakushauri kuhusu muundo wa biashara yako faida na hasara pamoja fursa mbalimbali
  2. Pili tutakufanyia utafiti na ushauri wa Jina la Biashara yako kwa kuzingatia vigezo vya SOKO
  3. Tutakufanyia Taratibu zote za usajili kuanzia Uandaaji wa Nyaraka Mpaka Kukamilika kwa Usajili Kampuni,TRA,Mashine za EFD na VFD,Vibali vya TBS pamoja na leseni
  4. Tutakuandikia Company Profile ya Kisasa kwa Lugha ya Kiingereza na Kiswahili
  5. Kama unahitaji mkopo kutoka katika taasisi za fedha tutakusaidia kufanya mchakato kwa kuzingatia mahitaji yako na vigezo vya taasisi husika.
  6. Tutakutengenezea Website ya kisasa kwa ajili ya Biashara na huduma zako.
  7. Tutakutengenezea, Logo, Business Card,Letter Head pamoja na Nyaraka nyingine za Kibiashara
  8. Tutakupatia Mfumo wa Kutunza kumbukumbu kwa njia ya Mtandao au kwenye Computer yako kwa ajili ya kusimamia Biashara yako
  9. Tutakufanyia Initial Marketing kwa Wateja wako (Inategemea aina ya biashara )wa Mwanzo ili kuwa na customer base ya kuanzia
  10. Pia tutakusaidia Mchakato wa Kufungua Bank Account kwa kutumia jina la Biashara yako (Deposit Ya Kwako)
  11. Tutakuwa nawe katika mchakato mzima wa kuendesha biashara yako mpaka itakapokuwa stable na wewe kupata uzoefu wa kutosha katika biashara yako.

Huduma hizi zinapatikana kwa pamoja au kwa moja moja na mfumo wetu wa malipo ni nafuu na unazingatia matokea katika kila hatua.Kama unahitaji huduma zetu wasiliana nasi kwa email:masokotz@yahoo.com au kwa simu +255710323060.
 
Back
Top Bottom