Vipimo vya presha vinanichanganya

Vipimo vya presha vinanichanganya

Charliemic

JF-Expert Member
Joined
Feb 17, 2019
Posts
602
Reaction score
969
Leo nimepima presha nimepata katika vituo vitatu tofauti majibu yamekuja tofauti tofauti.

Cha kwanza ilikuja 152/80/67 nikamwomba arudie ikaja 146/79/68.

Nikenda kituo cha pili nilipata 156/83/64 nikamwomba arudie ikaja 132/84/69 nikaenda kituo kingine nikapata 130/78/71.

Wataalamu naombeni ushauri wenu hapa napaswa kuanza tiba ya kushusha?

Sijisikii kuumwa, nipo normal.

Situmii pombe.
 
Una miaka mingapi?

Rudia mara tatu kwa siku tofauti.

Ofcourse usiwe suprised na Pressure kucheza haiwezi record same reading especially hizi digital.

Kikubwa kama Pressure iko Juu itabaki kuwa Juu tu
 
[emoji56][emoji56][emoji56][emoji56] Duhh hivi kumbe inakuwaga hivo mimi najua ile ya sehemu mbili mfano 140/90 sasa hii yakuwa na sehemu tatu sijawahi ona labda wajuzi waje kutuambia
 
Mkuu hunywi pombe bado una pressure aungekuwa unakunywa maana yake ungekuwa usha kufa.
Poleeee sana.
 
Una miaka mingapi?
Rudia mara tatu kwa siku tofauti.

Ofcourse usiwe suprised na Pressure kucheza haiwezi record same reading especially hizi digital.

Kikubwa kama Pressure iko Juu itabaki kuwa Juu tu
Umri miaka 35!
 
hivo vituo ulivoenda, wamekupima kwa Manually au Digitally ???

Embu jaribu kupima mara tatu au nne kwa siku tofauti tofauti ?.

Acha Pombe
Acha Sigara
Acha au punguza matumizi ya Chumv
Achana na vyakula vya mafuta
Usizidishe Lita 2 za maji yakunywa kwa siku.
Mazoezi
Achana Stress za Maisha joooh

Presha ni Muuaji wa kimyakimya.
 
Pressure ni vizuri kucheki ukiwa hujala kitu na unatakiwa ucheki dakika 10 baada ya kuwa umetulia,pia kwakuwa hiyo yako haiko juu sana, rudia kwa siku mbili tofauti muda uleule,ukiona ya juu inavuka 140 na chini juu ya 85 jua kuwa umeanza kupata shida ya pressure,then muone daktari ili akupime kujua chanzo cha hilo tatizo,kama ina haja ya kuanza dawa au uondoe visababishi bila ya kutumia dawa ili iweze kushuka...
 
Nimegundua kuwa makosa yalikuwa yanafanyika wakati wa upimaji ! walikuwa wanakosea uwekaji mkono! Mkono huwa unatakiwa uwe juu ya kitu mfano meza halafu iwe usawa wa moyo! Sasa mm waliokuwa wananipima nilikuwa nauweka kawaida usawa wa mwili!
 
hivo vituo ulivoenda, wamekupima kwa Manually au Digitally ???

Embu jaribu kupima mara tatu au nne kwa siku tofauti tofauti ?.

Acha Pombe
Acha Sigara
Acha au punguza matumizi ya Chumv
Achana na vyakula vya mafuta
Usizidishe Lita 2 za maji yakunywa kwa siku.
Mazoezi
Achana Stress za Maisha joooh

Presha ni Muuaji wa kimyakimya.
Kipi kinatoa majibu sahihi manual au dogital
 
Wasitumie digital hudanganya, watumie zile za zamani
 
Back
Top Bottom