Vipindi ya redio kugubikwa na matangazo ya kamari ni sawa?

Vipindi ya redio kugubikwa na matangazo ya kamari ni sawa?

Benderea

JF-Expert Member
Joined
May 25, 2021
Posts
686
Reaction score
1,303
Hii nchi sasa tunakoelekea mi naona siko!

Takriban radio zote zinachezesha kamari na ukifuatilia muda mwingi wa vipindi, niseme tu asilimia kubwa ya muda wao maudhui ni kamari. Je, tunajenga taifa la namna gani? Je, Serikali imeangalia inakuwaje hizi radio zinaruhusiwa kucheza kamari toka lafajir hadi usiku wa manane?

Je, Memorandum and articles of association za radio hizi zinaruhusu wamiliki wa radio kuchezesha kamari? Je, wana leseni za kuchezesha kamari? Brela kweli imetoa leseni kwa radio kuchezesha kamari? Je, hayo ndo malengo ya radio kuchezesha kamari?

Kwa kweli inanifikirisha sana haipiti dakika tano bila kusikia wasikilizaji wakihamasishwa kucheza kamari.

Je tunajenga taifa la aina gani?

Je, radio zimeshindwa kujiendesha mpaka zichezeshe kamari?

Mimi nadhani serikali inastahili kuingilia kati suala hili kabla halijaleta athari kubwa katika jamii yetu ikiwemo kupiga marufuku wenye radio kuchezesha kamari na kupiga marufuku maangazo yoyote ya radio moja kwa moja yahusuyo kupromote kamari.

Kama wanataka waanzishe kampuni za kamari na wasutumie radio kutangaza.

Mchelea mwana kulia hulia yeye.
 
Takriban radio zote zinachezesha kamari na ukifuatilia muda mwingi wa vipindi na niseme tu asilimia kubwa ya muda wao maudhui ni Kamari
Bunge lilikaa likatunga Sheria ya Kuchezesha Kamari alimaarufu km Michezo ya Kubahatisha na hio Michezo inaiingizia serikali Mabillion na Matrillion ya Shilling kila mwaka kwa hio ni ngumu hio michezo kufungwa maana ni moja ya pato la Taifa
 
Vijana huku kijjn hawana mpngo was kujituma kabisa wao kuboth or equal score
Serikali inachota Pesa kwenye hizo hizo both & equal score hapo hapo ukishinda 100 Million kwenye hii Michezo ya Kubahatisha basi jua 20 Million ni ya Serikali wewe utabaki na 80 Million tu kwa hio hizo promo Serikali haiwezi kuzizuia zisifanyike kwenye Radio na Tv maana inaziingizia Pesa nyingi Serikali
 
Ndugu, hili jambo lipo kwenye ilani ya chama cha mapinduzi ya 2015!! Sikumbuki ni kifungu gani ila lipo!! Tena wamesema kabisa “kuongeza idadi ya michezo ya kubahatisha kadri tunavyoweza”! Lengo ni lile lile la kuzalisha kizazi kinachotaka easy money na wajinga wawe wengi ili waendelee kutawala! Hivyo yani
 
Nadhani hii ni sehemu ya mapato ya redio nyingi kwasababu matangazo ya kawaida ya biashara tangu awamu ya 5 ianze sio mengi kwasababu ya hali ya uchumi wa nchi kwahiyo betting inasaidia kupata mapato
 
H
Nadhani hii ni sehemu ya mapato ya redio nyingi kwasababu matangazo ya kawaida ya biashara tangu awamu ya 5 ianze sio mengi kwasababu ya hali ya uchumi wa nchi kwahiyo betting inasaidia kupata mapato
ii ndiyo sababu watu wengi wameacha kusikiliza redio maana hakuna tena maudhui ya kujenga akili muda mwingi ni matangazo ya kamari tu.
 
Yaani unataka serikali ikose mapato, hizo kamali zipo kisheria kwa jina la michezo ya kubahatisha na hao wanaotangaza ni sehemu ya kuendeshea vipindi vyao
 
Hii nchi sasa tunakoelekea mi naona siko!

Takriban radio zote zinachezesha kamari na ukifuatilia muda mwingi wa vipindi, niseme tu asilimia kubwa ya muda wao maudhui ni kamari. Je, tunajenga taifa la namna gani? Je, Serikali imeangalia inakuwaje hizi radio zinaruhusiwa kucheza kamari toka lafajir hadi usiku wa manane?

Je, Memorandum and articles of association za radio hizi zinaruhusu wamiliki wa radio kuchezesha kamari? Je, wana leseni za kuchezesha kamari? Brela kweli imetoa leseni kwa radio kuchezesha kamari? Je, hayo ndo malengo ya radio kuchezesha kamari?

Kwa kweli inanifikirisha sana haipiti dakika tano bila kusikia wasikilizaji wakihamasishwa kucheza kamari.

Je tunajenga taifa la aina gani?

Je, radio zimeshindwa kujiendesha mpaka zichezeshe kamari?

Mimi nadhani serikali inastahili kuingilia kati suala hili kabla halijaleta athari kubwa katika jamii yetu ikiwemo kupiga marufuku wenye radio kuchezesha kamari na kupiga marufuku maangazo yoyote ya radio moja kwa moja yahusuyo kupromote kamari.

Kama wanataka waanzishe kampuni za kamari na wasutumie radio kutangaza.

Mchelea mwana kulia hulia yeye.
Kwamba...
1. Yaani mtu aanzishe redio kwa pesa zake huku akiwa amefuata taratibu zote za uanzishwaji wa redio..!!

2. Mtu huyo anatangaza kamari/michezo ya kubahatisha uliyopitishwa na bunge (mbunge wako akiwemo, hivyo wewe umepitisha)..!!!

HALAFU LEO UNAKUJA VYOKO VYOKO, VYOKO VYOKO..!! Anza na mbunge wako kwanza
 
Back
Top Bottom