Vipo wapi vyombo vya habari vya Tanzania kwenye Press conference ya Mbowe? Ishukuriwe mitandao ya kijamii

Resilience

JF-Expert Member
Joined
Jan 4, 2023
Posts
1,096
Reaction score
4,948
Hadi waigizaji na wanamziki wanaajiriwa na kulipwa fedha nzuri na wamiliki wa vyombo vya habari ni kwa sababu waliosomea hii kazi wameacha taaluma na kuishi kwa kuambiwa na kufikirishwa.

Leo hii waandishi wa habari wanalipwa elfu 30 hadi 50 na hii ni kwa mujibu wa RC Mara.Kinyume na hapo hawaji kwenye press iliyoitisha. Jiulize leo kama wamekuwa cheap to this amount wanapeleka wapi Tqsnia?

Tumeshuhudia wengi wao hadi wanastaafu hawana nyumba na watoto wao bado wanasoma maisha duni. Haya yote yametokana na ukweli kwamba waandishi na wahariri wa habari Tanzania hakuna. Mfano kwa sasa mtangazaji mwenye uthubutu wa kuhoji bila biasness amebaki mmoja yupo star TV medani za siasa. Waliobaki wote hana uwezo wa kuhoji au kuvuna jambo tangible kwa mhojiwa.

Je, hatuoni kwamba siku za usoni tutaajiri watangazaji kutoka Kenya? Hatuoni kwamba fursa za kutoa watu kwenda mashirika makubwa ya utangazaji Duniani zitaondoka na kuchukuliwa na Mataifa jirani?

Tasnia imebaki na vipindi vya michezo na kuripoti yale tu watawala wanayosema.....not good oohooooo
Mwandishi kwenye habari za kimataifa anacopy na kupaste kilichoripotiwa na vyombo vya nje....hakuna uchambuzi binafsi.
 
Mfano kwa sasa mtangazaji mwenye uthubutu wa kuhoji bila biasness amebaki mmoja yupo star TV medani za siasa. Waliobaki wote hana uwezo wa kuhoji au kuvuna jambo tangible kwa mhojiwa.
Wapo wawili pale sio mmoja angalia vizuri, medani za siasa (Chief Odemba) na kile kingine cha yule jamaa walisema ametimkia Azam kumbe ni tetesi tu

Pia kipo kingine cha Channel Ten nacho kinapiga misumali uwe unaangalia vizuri kinaonyeshwa mida ambayo watoto wameshalala 4 kuelekea 5
 
Mkuu Resilience , kwanza japo umetusema vibaya sisi waandishi wote wa habari na sekta yote, ila sio wote, bado tunao the few good ones, ila hawavimi, lakini wapo, mmoja yupo Channel Ten, anaendesha kipindi cha KMT, kinarushwa kila siku za Jumapili Saa 3:00 usiku, ila maoni yako ni ukweli mchungu kumeza lakini huu ndio ukweli!.

Pili ni Chadema wenyewe, usikute hawakuwaalika rasmi the mainstream media. Media tusipoalikwa hatujiendei tuu.

Tatu, it's high time, Chadema wawe na media yake, toka alipoondoka Tumaini Makene, ofisa habari wa Chadema, Chadema Haijawahi kuwa na ofisa habari wake.

Mwisho sometimes ni Chadema wenyewe na inferiority complex to shy away from the media. Angalia kilichotokea hapa Uchaguzi 2020 - Je, Tanzania tuna upinzani makini, upinzani wa kweli wa kuing'oa CCM madarakani au bado sana? Nilichoshuhudia leo uzinduzi CHADEMA, kiukweli... kwa faida ya wavivu kufungua links
P
 
Mmmh!
 
Uzuri ni kwamba 95 % ya Watanzania hawahangaiki na vyombo hivyo , ukiwaona kwenye TV jua wanaangalia soka
 
Pascal unajitahidi kuandika ila upo subjective sana linapokuja swala la ccm vs wengine hasa chadema.
Inamaana kwa miaka yote hiyo hao chadema wasijue namna ya kupata milage?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…