CalvinKimaro
JF-Expert Member
- Sep 11, 2017
- 245
- 314
Awali ya yote niwape pole wale wote watakaofuata agizo la kutoshiriki uchaguzi kwa kutopiga kura.
Watakuwa kwa hiyari yao wenyewe wamejinyima haki yao. Hakuna mwingine atakayeumia isipokuwa wao wenyewe na chama chao.
Nadhani CHADEMA wanadhani kwa kususa mpango wao wa kuonyesha kuwa TANZANIA kuna Chama kimoja utafanikiwa. Ukweli ni kwamba huenda wakajikuta ni wao peke yao ndio wamesusa. Watakuta kura inashirikisha vyama vingi. Hata ACT kususa sijui!
CHADEMA keshajua karibuni hakitakuwa chama kikuu cha upinzani! Nafasi hiyo itachukuliwa na ACT na ki na ZITTO wanajua!
Ukiwasikiliza kina mbowe, Jacob, Lema na wenzao utabaini kuwa wanadhani wataweza kususia local government! Ni kujidanganya kulekule!
Hivi tuseme local government imeleta maji au umeme mtaani ni nani mjinga atasusia kwa kuwa tu Mbowe kasema? Au tuseme mtaani kumeingia kipindupindu Serikali ya mtaa ikapiga marufuku kupika na kula magengeni?
Mama ntilie atapika akiulizwa adai hatoi ushirikiano kwa serikali ya mtaa? Itokee Serikali ijenge shule au zahanati unataraji mtu asusie huduma ya elimu na matibabu kisa Lema au Jacob kasema?
Mtu atakataa kulipa kodi adai hataki kutoa ushirikiano na serikali? Si atafungwa?
Hivi viongozi wenye akili zilizopauka hivi ndio tuwape Ikulu?
Mbowe anadai hataki kwenda kufungua shauri mahakamani eti kwa kuwa anahesabu hakuna uchaguzi hivyo hajui ashitaki nini? Kweli? Sio hawa wamefanya Kisutu makazi yao kwa kufungua na kufunguliwa kesi pale? Leo anapaogopa?
Hivi kweli wana ushahidi au ni mpango wao toka awali? Chadema wawe na ushahidi lakini wakatae kuupeleka Kisutu? Mbona haielekei? Hawa hawana ushahidi!
Lakini hivi wamewaza implications za wao kususa? Wanajua hasara ya kukosa kushiriki local government? Hawajui ni kujitenga au kujiweka mbali na wapiga kura? Watawezaje kudhibiti mapato na matumizi ya serikali? Watapiga ramli?
Je wamefikiria implications kwa uchaguzi mkuu ujao? Watashiriki? Si itakuwa kichekesho? Sawa mtoto agome kwenda vidudu asubiri Hadi afikie umri wa kwenda chuo kikuu ndio ajifanye anapenda kusoma!
Na ikiwa watashiriki wana uhakika upi kuwa haya makosa ya sasa hayatajirudia oktoba 2020?
Hivi wabunge wenu watakubali msusie? Mawe! Mtashiriki hivyohivyo! Sawa mbuzi vingunguti kila mmoja anadhani mwenzie ndio atachinjwa yeye atapona!
Kuna jambo moja kubwa linawadaa! Kudhani wana nguvu ya umma! NI mpaka watakapotambua adui yao ndiye ana nguvu ya umma na ya dola ndipo watakapopanga mambo Yao uzuri.
Ukweli ni kwamba kwa nguvu ya umma na ya dola iliyonayo CCM ni kujidanganya kudhani eti nchi itasimama siku ya kura au mamilioni ya watu watamwagika mabarabarani kufanya vurugu!
It's just a matter of time! Uchaguzi utafanyika kwa amani na utulivu. Serikali zote 2 za mitaa na Serikali kuu zitafanya kazi huku nyie mkilalamikia ndani ya visanduku vya Twitter!
Mtagombana wenyewe kwa wenyewe!
Uamuzi huu ndio umeweka wazi udhaifu wa Mbowe kiuongozi! Time to change him otherwise....!
Tanzania na watanzania wamebarikiwa amani! Hamna wa kufanya wauane.
Ushauri wangu kwa kina ACT, TLP, NCCR, NLD, CUF na wenzao msiige huu upuuzi. KUFA KUFAANA!