Kipala umekuja kujiunga na Lugha, na mambo ya Dini na imani umekimbia nenda kanisani ukafundishe Yesu Mwana wa Mungu Yesu Mwokozi wetu tuache hapa Kipala chako kinafanya kazi kweli kweli.
Neno hilo Virus vya Computer au Virusi vya ukimwi liache kama kawaida enategemea mtu atakavyo litumia hilo neno la Virusi vya Computer au Virusi vya ukimwi, unajuwa kirusi kimoja cha Computer kinazaa virusi vingi ndani ya hiyo Computer? kaulize kule Technology & Science Forum kaulize hilo swali utapata jibu lake.
Hakuna ubaya wowote kusema kuwa Computer yangu imevamiwa na Virusi ndani yake. Au kusema kuwa Mtu fulani ana Virusi vya Ukimwi ni sawa saw tu na kusema kuwa Computer yangu imevamiwa na kirusi haifanyi kazi.
Umeshaleta Topic mpya Neno Video ni neno la Kiingereza hakuna kwa kiswahili Tafsiri ya neno Video litakwenda hivyo hivyo Video tu.na neno Virus ni neno la kiingereza tunaweza kusema kwa lugha yetu ya kiswahili kuwa ni Virusi kwa wingi tu au Kirusi kwa umoja hakuna matatizo itategemea vile utakavyotumia wewe .Asante kwa kutupa mahubiri ya kidini hata hapa. Usiwe na wasiwasi, kuna uwezekano ya kwamba nimekutangulia kidogo hapa lugha (sifiki mara nyingi)
Sasa tuache uchungu.
Naomba nisaidie: nikielewa vema unasema umoja ni Kirusi na uwingi ni Virusi . Nimeelewa sawa?
Lakini
a) Kirusi ni lugha. Tutofautishe kivipi?
b) Neno la nje ambalo limepokelewa katika Kiswahili ni "virus", siyo "kirus".
c) unasema ni sawa kuandika "Mtu fulani ana Virusi vya Ukimwi". Je hii inataka kusema ameambukizwa na virusi 1 au vingi/nyingi?
Kuna sababu gani kutumia "virusi" tofauti na "video" ?
Mkuu nakubaliana na wewe kwa lugha yetu ya kiswahili ukianza na herufi ya (Vi) basi ina maanisha ni wingi wa kitu aidha chakula au kitu chochote chenye kuwa na wingi ndio maana tukatumia herufi ya (Vi) kwa mfano chakula ni umoja wingi wake ni vyakula, chombo ni kimoja vyombo ni vingi,Kisahani ni kimoja Visahani ni zaidi ya kimoja. Hiyo ni baadhi ya mifano michache tu niliyokutolea ipo mingi tu asante mkuu wikama kwa ufafanuzi wako mzuri.navyojua katika lugha ukianza na Vi - basi wingi wake ni vya na ukianza na Ki- inaenda na cha-, mfano kiti wingi wake ni viti, kwa kuwa neno la virusi ni kingereza yaani VIRUS, linatumika katika kiswahili basi lifuate kanuni za kiswahili yaani ni virusi vya ukimwi na siyo virusi ya ukimwi kikiwa kimoja kirusi cha ukimwi nadhani hii itasaidia .
Jamani neno "virusi" limeingia katika lugha.
Wengu huandika "Virusi vya UKIMWI", "virusi vya kompyuta".
Lakini hii ina matata. Nimeshaona watu wanaoandika "virusi vya kompyuta ni hatari; wiki iliyopita kirusi kipya..."
Hii inaonyesha udhaifu wa kawaida hii;: namna gani kutofautisha kati ya virusi 1 (virusi kimoja? virusi vimoja ????) na virusi 100 (virusi vingi?).
Mimi naona afadhali tukubaliane "virusi" ni neno la Kilatini kilichoingia hapa kupitia Kiingereza na kama maneno yale mengi tuseme
virusi ya kompyuta, virusi ya UKIMWI kama ni 1
virusi za kompyuta nyingi ....
Mnaonaje ?
Kama unaweza kukikamata kirusi kimoja, then unasema Kirusi cha, kama unamaana ya aina moja ya kirusi, pia unaweza kusema kirusi cha HIV kama unavyoweza kusema kinywaji cha pepsi. Pia unaweza kusema virusi vya HIV. Lakini kamwezi huwezi kusema virusi cha HIV, haitakuwa sahihi kwa kufuatisha ngeli za kiswahili.
Usichanganye vi ya Kiswahili na ya kiingereza, katika kiingereza hawa wadudu wanaitwa virus, jina linaanza na vi, katika kiswahili vi inaashiria wingi, na kimoja hakiwezi kuitwa virusi cha, kinaitwa kirusi cha kwa kufuatisha ngeli za Kiswahili...
Kirusi (n)Ila tu kwa "virusi" - naona ugumu kwa sababu "Kirusi" ni lugha.
Asante nimeelewa hoja lako.
Lakini naomba jibu swali linalofuata:
Je tukitazama filamu nyingi za video tunatazama pia filamu 1 ya kideo?
Nadhani hatuwezi, tunasema video moja, video nyingi si vingi; video ndefu si virefu n.k.
Sasa video sawa na virus ni maneno ya kigeni yaliyopokelewa katika Kiswahili. Mara nyingi maneno haya yanafika katika ngeli ya n-n (i-zi).
Si lazima, maana kuna njia nyingi za "kuswahilisha" neno la kigeni (kama dokta - madokta si wadokta wala dokta wengi).
Ila tu kwa "virusi" - naona ugumu kwa sababu "Kirusi" ni lugha.
Kwa sababu gani virusi iwe tofauti na video? Kwa nini tusiseme virusi moja - virusi nyingi ?
Asante sana kwa mchango - umeikuta wapi? Au umeitunga mwenyewe?Kirusi (n)
- lugha yenye asili ya KiSlaviki katika familia ya Indo-European inayozungumza na watu wa Urusi, Belarus, Ukraine, Kazakhstan na Kyrgyzstan na mataifa mengine jirani
- umoja wa 'virusi'
Ukiangalia kwa undani utagundua neno "virus" halijatoholewa moja kwa moja kutoka Kiingereza na kuongezewa i ya mwisho kupewa sauti ya kiswahili tu, matamshi ya Kiingereza ni "vairas" na kiswahili ni lugha ya matamshi inayotohoa kwa matamshi kuliko maandiko, kwa hiyo kutohoa moja kwa moja kungekuwa "vairasi"....
Kwenye lugha ya kiswahili kuna maneno mengine haya wingi! mf: Maji, Virusi, bamia, mchele, unga n.kKwa maoni yangu kuna utata unaotokana na kutoholewa kwa neno virus kuwa virusi. Ile "vi" katika virusi sio yakuashiria wingi ila ni sehemu ya jina lile. Kipala asema kweli kuwa hakuna neno kam "Kirusi". Shida kuu nikupata wingi wa virusi moja ambapo naonelea iwe "Mavirusi mengi".
Una uhakika "Virusi" iko katika kundi hili cha maneno yanayojumlisha kiasi lakini hayawezi kuhesabu jambo?Kwenye lugha ya kiswahili kuna maneno mengine haya wingi! mf: Maji, Virusi, bamia, mchele, ungan.k
Katika neno Virusi hakuna wingi wala umoja!Una uhakika "Virusi" iko katika kundi hili cha maneno yanayojumlisha kiasi lakini hayawezi kuhesabu jambo?
Maana maji ni jumla; tunaweza kuwa na maji mengi au kidogo, lakini hatuna maji 1,2,3 yaani hatuna umoja kilugha; badala yake tunaweza kuhesabu matone ya maji. Vivyo hivyo mchele: kilugha haina umoja, tunaweza kuhesabu aina au punje za mchele lakini haiwezekani kutaja mchele 1,2,3.
Kwa virusi inawezekana kuzihesabu 1,2,3 (estimate of virusload).