Analogia Malenga
JF-Expert Member
- Feb 24, 2012
- 5,108
- 10,191
Uchunguzi wa BBC umebaini kuwa aina mbili za dawa ambazo zilitumika kutibu wagonjwa wa corona nchini India - remdesivir na tocilizumab - zimekuwa zikiuzwa katika soko la magendo kwa bei ya juu ndio maana kuna upungufu mkubwa sana wa dawa hizo.Mwandishi wa BBC, Pandey anaripoti kutoka mji mkuu wa India Delhi.
Mjomba wake Abhinav Sharma alikuwa na homa kali na alikuwa anapata tabu kupumua wakati alipolazwa hospitalini huko Delhi.
Alikutwa na virusi vya corona na madaktari waliiambia familia yake itafute dawa aina ya remdesivir - dawa ambayo imeruhusiwa kwa ajili ya matibabu ya corona wakati wa dharura nchini India ",hii ikiwa ina maana kuwa madaktari wanaweza kutoa ruhusa ya matumizi ya dawa hizo kwa kutokana na sababu maalum.
Lakini upatikanaji wa dawa hiyo umeonekana kuwa jambo ambalo haliwezekani - dawa ya 'remdesivir' imeadimika na haipatikani kokote.
Bwana Sharma alihangaika kuwapigia watu kumsaidia kupata dawa ya kumsaidia mjomba wake ambaye hali yake ilikuwa inazidi kuwa mbaya kila saa.
"Nilikuwa na machozi machoni mwangu. Mjomba wangu alikuwa anapambana na maisha yake na nilikuwa nahangaika kupata dawa ambayo ingeweza kuokoa maisha yake," alisema.
"Baada ya kupiga simu kadhaa, nililipa mara saba ya gharama halisi ya dawa nilikuwa radhi kulipia gharama yoyote ile kwa kweli, lakini nawaonea huruma watu wale ambao hawana uwezo wa kununua kwa gharama hiyo," alisema.
Changamoto aliyokabiliana nayo Bwana Sharma, inazikabili familia nyingi sana mjini Delhi, ambapo watu wengi huwa wanahangaika na kufanya lolote ili kuokoa maisha ya wapendwa wao.
Baadhi wanasema huwa wanalazimika kulipa gharama kubwa sana kwa ajili ya dawa hiyo - wengi huwa wanaishia kwenye soko la zamani la dawa la mjini Delhi.
Aliongeza kuwa kiwanda kilikuwa kinafanya kazi kwa nguvu zote ili kufikia mahitaji ya wwagonjwa lakini hili soko la magendo linawarudisha nyuma".
"Tunaelewa maumivu wanayoyapata watu. Hawapaswi kuambiwa kwenda kutafuta dawa. Tunaamini kuwa ongezeko la uzalishaji wa dawa katika siku chache za mbeleni kunaweza kufanya hali iwe nafuu kidogo."
Wauzaji katika maduka ya dawa wanasema hawana wasambazaji wa dawa pia.
"Mwanamke mmoja kutoka Hyderabad wiki iliyopita, baba yake alikuwa hospitalini mjini Delhi - alisema angeweza kulipia kiasi chochote cha fedha kupata dawa hiyo.
Lakini nilikuwa sina cha kufanya ," alisema Rajeev Tyagi, makamu wa rais waa jumuiya ya wanasayansi wa Ghaziabad waliopo karibu na Delhi.
Lakini ilikuwaje dawa hiyo ilifika katika soko la zamani la dawa Delhi?
Mkurugenzi wa jumuiya zote za madawa nchini India (All India Chemists and Druggists Association) Bwana, Rajiv Singhal,- chombo ambacho kinakutanisha wamiliki wote wa maduka ya dawa - wamekanusha kuwa wamiliki wa maduka hawahusiki.
"Nina uhakika kuwa hakuna mwanachama wetu ambaye anahusika na vitendo hivyo. Hii ni dharura ya afya kitaifa na hivyo nataka kutoa ujumbe ulio wazi kabisa kuwa hatua kali zitachukuliwa kama mtu yeyote atabainika kuhusika akiuza dawa hizo kinyume na sheria " alisema.
Lakini suala hili linaonekana kwamba si kwa dawa ya remdesivir peke yake. Gharama imeongezeka dawa nyingine za kuokoa maisha kama tocilizumab, gharama yake imepanda pia.
Dawa ambazo zimekuwa zikiuzwa kama Actemra zimeonyesha matokeo chanya kwa wagonjwa mahututi duniani kote.
Wataalamu wanasema utafiti zaidi unahitajika ili kuelewa ufanisi wake ingawa hospitali nyingi zimeripoti kuwa dawa hizo zinafanya kazi vizuri.
Lakini dawa hiyo ilikuwa imetengenezwa kwa ajili ya wagonjwa wa mishipa na mgongo 'rheumatoid arthritis' na wasambazaji wake huwa wanatambuliwa.
Cipla inauza dawa nchini India kwa niaba ya Roche iliyoko Switzerland- na huwa inaagizwa yote.
Lakini ni vigumu kuipata haswa ukiwa unaihitaji ndani ya saa kadhaa.
Muwakilishi wa Cipla kaskazini mwa India alisema dawa hiyo imekua ikihitajika sana katika wiki za wiki za hivi karibuni.
"Tumeongeza usambazaji lakini tunatarajia uhitaji utaongezeka katika siku zijazo,"alisema.
BBC iliweza kubaini kuwa kuna matukio kadhaa ambapo hospitali zilikuwa zinawataka ndugu wa wagonjwa kujitafutia dawa wenyewe ili kuokoa maisha ya wapendwa wao.
"Nilienda maduka ya dawa zaidi ya 50 mjini Delhi. Maduka yote walihaidi lakini lakini walihaidi kunipa dozi mbili au tatu kwa bei tofauti kwa kila dawa.
Ilinichukua siku mbili kupata dawa ambayo shangazi yangu alikuwa anaihitaji," alisema mkazi wa Delhi, ambaye hakutaka jina lake litajwe.
Lakini muwakilishi wa Cipla alikanusha kuwa dawa aina ya tocilizumab, ilikuwa inauzwa katika soko la magendo.
"Tunafuatilia kila dawa tunayoitoa ili kuhakikisha kuwa, hakuna ulaghai wowote unaojitokeza. Hatutaki ulaghai kama huo kutokea,"alisema.
BBC Swahili