Analogia Malenga
JF-Expert Member
- Feb 24, 2012
- 5,108
- 10,191
Rais wa Uganda Yoweri Museveni ameruhusu waendesha boda boda na texi kuwabeba abiria kwa masharti kwamba lazima wavae barakoa kuzingatia muongozi wa kuzua maambukizi ya corona.
Rais pia alipunguza muda wa kafyu kwa saa mbili - sasa itaanza saa tatu usiku saa za Afrika Mashariki.
Katika hutuba yake kwa taifa iliyorushwa moja kwa moja kwenye runinga usiku wa Jumanne, Bw. Museveni pia aliruhusu kufunguliwa kwa saluni na baadhi ya maduka makubwa yanazingatia viwango vya afya. Vyombo vya Habari nchini humo viraripoti kuwa maduka 110 syamefikia masharti yaliyowekwa.
Pikipiki zinazojulikana kama boda boda zitaruhusiwa kufanya kazi hadi saa kumi na mbili jioni kuanziaJulai 27.
Rais Museveni hata hivyo amesema shule na maeneo ya kuabudi yataendela kufungwa.
Amesema mabadiliko hayo yamefikiwa kufuatia ushauri kutoka kwa wanasayansi.
Awali wahudumu wa boda boda waliruhusiwa kubeba bidhaa pekee yake kwa kuhofia itakua vigumu kwa abiria na muendeshaji piki piki kutukaribiana.
Waendeshaji boda boda waliishitaki serikali kwa kupiga marufuku biashara yao wakisema hatua hiyo imewaathiri kiuchumi.
Uganda kufikia sasa imethibitisha kuwa na watu 1,072 waliambukizwa virusi vya corona. Hakuna mtu yeyote aliyefariki kutokana na ugonjwa wa corona.
Hivi karibuni Uganda ilifungua sehemu ya mpaka wake kwa maelfu ya wakimbizi wa kutoka nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo waliokuwa wamekwama katika eneo hilo kwa zaidi ya mwezi mmoja.
Karibu watu 3,000 walitoroka makwao mwezi Mei baada ya mapigano ya kijamii kuzuka katika mkoa wa Ituri kaskazini mashariki mwa DRC.
Lakini hawakuweza kuvuka na kuingia Uganda kwa sababu ilikuwa imefunga mipaka yake mwezi Machi kama juhudi za kudhibiti maambukizi ya virusi vya corona.
Uamuzi ulifikiwa kwamba wakimbizi hao watawekwa karantini kabla ya kupelekwa kambini.
Hili litafanyika katika muda wa siku 14 katika kituo cha kuwatenga watu kilichopo kilomita 13 sawa na (maili nane) kutoka mpakani.
Shirika la Umoja wa Mataifa la kushughulikia wakimbizi (UNHCR) limesema kuwa litawafanyia uchunguzi wa kimatibabu watu hao kubaini ikiwa baadhi yao wameambukizwa virusi vya corona.
Kufikia sasa wakimbizi 52 wamepatikana na virusi vya corona nchini Uganda katika karibia 900 waliothibitishwa kupata maambukizi.
BBC Swahili