Sildenafil Citrate
JF-Expert Member
- Jan 29, 2021
- 577
- 2,595
Ni mzizi ulio na faida kubwa sana kwa afya. Vyanzo vya kihistoria vinataja asili ya mzizi huu kuwa ni Kusini mwa bara la Asia.
Hupatikana kwenye familia kubwa ya Zingiberaceae.
Kwa mujibu wa USDA, tangawizi ni mzizi ulio na mjumuiko wa nishati, protini, wanga, nyuzilishe, madini chuma, calcim phosphorus, magnesium, zinc, selenium, vitamini C, B6, B12 na folate.
Tangawizi huwa pia na kemikali hai za kampaundi za phenolic na terpene ambazo mfano wake ni gingerols, shogaols na paradols.
Unaweza kutumia kama chai, unaweza kutafuna au pia inaweza kuongezwa kwenye mapishi ya chakula kama sehemu ya viungo.
Chanzo: Afyainfo

- Hutibu tatizo la Kiungulia na kutapika kwa wanawake wajawazito, wenye matibabu ya saratani na wale wanaotapika wawapo safarini
- Kemikali za gingerol ambazo hupatikana kwa wingi kwenye tangawizi mbichi huwa na uwezo wa kukinga pamoja na kudhibiti ukuaji wa aina mbalimbali za seli za saratani mwilini.
- Huharibu sumu mwilini, kulinda seli za mwili pamoja na kuzuia au kutibu aina mbalimbali za uvimbe.
- Tangawizi huongeza uzalishwaji wa vichocheo vya kiume, hupunguza uharibifu wa kuta za ndani ya korodani, huondoa sumu pamoja kupanua mishipa ya damu inayoelekea kwenye uume.
- Ni dawa nzuri ya kikohozi na mafua. Tangawizi hufungua mfumo wa hewa pamoja na kupunguza uzalishwaji wa ute unaoziba mfumo huu. Huwa pia na sifa ya kupambana na aina mbalimbali za virusi wanaosababisha mafua, pamoja na kuongeza uimara wa kinga mwili.
Unaweza kutumia kama chai, unaweza kutafuna au pia inaweza kuongezwa kwenye mapishi ya chakula kama sehemu ya viungo.
Chanzo: Afyainfo