Visa mbalimbali kuhusu kukosa uaminifu kwenye pesa.

Visa mbalimbali kuhusu kukosa uaminifu kwenye pesa.

Ziltan

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2011
Posts
2,672
Reaction score
6,880
Habari ndugu wanaJF,
Kwa Leo naomba nianze na Visa viwili,
Ingawa vipo vingi nilivyoshuhudia kuhusu watu kukosa uaminifu kutokana na mambo ya fedha,
1.mwaka 2004 nikiwa chuoni wilaya fulani, tukiwa tunaelekea kuhitimu, tukapanga kufanya mahafali, akawa amechaguliwa mwenzetu mmoja kuchangisha fedha,
Zoez likaendelea, alipotakiwa kuwasilisha fedha ili maandaliz yaendelee, jamaa akawa hana karibia nusu ya fedha, kuja kufatilia kumbe alipoanza kuchangisha alipata demu pale chuoni na alitumia gharama kubwa sana kwa huyo demu,
Jamaa alishindwa kulipa hizo hela akaishia kufukuzwa chuo, na kupoteza nafasi ya kuajiriw kiulaini serikalini, maan ilikuwa tunamaliza Novemba halafu mwezi March mwaka unaofata tunaingia kazini.
2.kuna mzee mmoja wilaya ya Chato, alikuwa na kijana wake yupo Mererani,
Huyo mzee alikuw mgane na alikuwa akiishi na wajukuu zake wawili, vijana walikuw washakuwa wakubwa wote na washatoka kwenda kutfta na wengine kuolewa,
Sasa huku na huku kwa kujibana yule kijana wa mererani akawa amepata kiasi cha shilingi Milion 40,
Akaona aitume nyumbani kwa mzee, ili asaidie kusimamia ujenzi pale nyumbani walau wapate hata pa kufikia, maana pale nyumban hali ni Taabani, yaani nyumba ni mbavu za mbwa kuingia ndani mpaka uiname, hali tete.
Basi kijana akafanya mawasiliano na babaake, hela ikatumwa.
Mzee kuipata hela akaanza kutumbua tu,
Hadi akaoa kigori, unaambiw mzee alikuw anahemea kilo za nyama, mifuko ya ngano, sukari anachukua mifuko mizima anaweka ndani,nk
Yaan kifupi mzee alijulikana pale mtaani kuwa anamilik hela,
Huku na huku wajanja wakamwingia kukopa hela, mzee akatoa Sh 15M kwa maelezo yake aliyoyatoa mahakaman, maan alianza kudai bila mafanikio hadi wakafikishana huko.
Huku kijana akarudi nyumbani kuja kuangalia ujenzi wa nyumba, aliyoyakuta hakuamini.
Alichokifanya Siku moja wameamka asbh, pale nyumbani walikuwepo watu watatu, yaani yeye kijana, huyo mzee pmj na mjukuu,
Alichokifanya jamaa aliagiza kale katoto dukani,
Huku nyuma akashika babaake, akachinja kama kuku, kisha kutoweka pasipojulikana hadi Leo.
Wananzengo hawakushangazwa sana na hicho kitendo zaidi walisema afadhali amemkomesha kwa maana mzee alizingua sana.
Mtanisamehe mimi sio msimuliaji na mwandishi mzuri ila naamini uzi huu, utakuw fundisho kubwa kuhusu mambo ya fedha.
Karibuni kwa visa zaidi ili kuelimishana na kupata tahadhari,
Mimi vipo visa vingi ntaendelea kuleta kadri muda utakavyo ruhusu.
 
Karma is real ,ukifanya mambo ovyo juu ya pesa na haki ya mtu hufiki popote utateseka tu.
 
Back
Top Bottom