Visa na visanga vya misibani

Visa na visanga vya misibani

TheDreamer Thebeliever

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2018
Posts
2,490
Reaction score
3,584
Habari wadau!

Kuna tabia za ajabu sana siku hizi, watu hawana utu ukifa kwao sherehe.

Mzee alipofariki, rafiki yake wa karibu alipewa jukumu la kwenda kutafuta mahali pa kuchimba kaburi, kwa wasiojua hata maeneo ya kuzikia pale makaburini yana madaraja na bei ni tofauti. Best yake kabisa mshua akapewa pesa akalipie daraja A yeye akaenda kumtupa mzee daraja la mwisho kabisa huko akapiga cha juu.

Alipofariki bro kuna mjomba alichangisha 2 Million kwa washikaji na wafanyakazi wa marehemu akaleta 600k nikatafuta daftari la mchango nikalipata mbona palichimbika.

Ebu tupe kisanga chako cha msibani kama unacho tucheke😂😂

1627668162691.png

 
Aya ya pili inatufundisha kujitahidi kuyaishi maisha yetu tuiwa hai.

Imagine hapo unaenda kaburini bado hujafika makazi ya “mpiga zumari” wa zamani, umefika umechoka unakutana na foleni ya wenzako wanasubiri kushughulikiwa kwa mikia ya taa utoke hapo ukageuzwe kuni sasa😁😁
 
hujawahi kusikia zamani wafalme walizikwa na making zao + watu wa kuwalinda...unaambiwa watu walikuwa wanagombania kwende kuzikwa na mfalme
Mkuu acha uongo bana yaani mtu ameshakufa , kisha akagombanie kuzikwa kwa mfalme tena, kwel tena na hiki ni kituko cha msibani aisee , hebu nieleze anaanzaje anzaje kwenda kugombania kuzikwa pahala alipozikwa mfalme , huku yeye ameshakufa
 
Kule kwetu alifariki mama mmoja, alikua anazo anazo. Miradi yake ilikua ni pamoja na guest house ya vyumba 25, kuku 600 wa nyama na mayai pamoja na ng’ombe.

Siku ya karamu ya msiba wake, walichinja kuku kama 50, ng’ombe mmoja. Kulikua na buffet la ndizi nyama, wali mweupe, pilau, kuku chips. Kuku mchuzi. Kila mtu alipata soda moja.

Ule msiba mpaka leo unazungumziwa huku kwetu Kwamtogole.
 
Back
Top Bottom