#COVID19 Visa vipya 21 vya COVID19 vyaongezeka. Jumla ya visa yafikia 248

#COVID19 Visa vipya 21 vya COVID19 vyaongezeka. Jumla ya visa yafikia 248

Influenza

JF-Expert Member
Joined
Jul 1, 2018
Posts
1,509
Reaction score
3,756
Wizara ya Afya Uganda imetangaza ongezeko la Wagonjwa 21 wote wakiwa raia wa Uganda na wamepatikana baada ya sampuli 1,071 kupimwa katika mipaka ya nchi hiyo

Wagonjwa hao wamepatikana katika mipaka ya Elegu (Visa 17) na Mutukula (Visa 3) na Malaba (Kisa 1). Pia, sampuli 253 za kutoka katika mitaa ya Uganda zimepimwa na kukutea hazina maambukizi

Aidha, Wizara hiyo imetoa tahadhari kuhusu taarifa potofu inayohusu Madereva 105 wa Malori waliokutwa na maambukizi iliyotolewa jana na akaunti ya Mtandao wa Kijamii uliojifanya kuwa Wizara ya Afya. Imetahadharisha kuwa jana haikutoa taarifa za #COVID19

Wizara imesisitiza kuwa madereva wote watakaoingia #Uganda watapimwa na Madereva wageni wataokutwa na maambukizi watarudishwa nchini kwao na Waganda watapelekwa katika Vituo mbalimbali vya Afya nchini humo

photo_2020-05-18_12-21-10.jpg
 
NNadhani Nairobi na Mombasa bado wana nyanya na karoti za kutosha, ila zikiisha utasikia madereva kutoka Tanzania wamepimwa hawana corona, tusubili si mbali.
 
Back
Top Bottom