Visa vipya 43 vya COVID19 vya madereva wa malori vyathibitishwa Uganda. Wapo Watanzania Watano

Visa vipya 43 vya COVID19 vya madereva wa malori vyathibitishwa Uganda. Wapo Watanzania Watano

Influenza

JF-Expert Member
Joined
Jul 1, 2018
Posts
1,509
Reaction score
3,756
Jana, Mei 15, 2020 Uganda imetangaza visa vipya 43 vya #COVID19 vimeongezeka na vyote vikiwa ni vya Madereva wa Malori na kufanya jumla ya visa kufikia 203

Wizara imesema jumla ya sampuli 2,558 zimepimwa kati ya hizo; 1,838 ni za Madereva wa malori na 720 ni za Wakazi wa Uganda ambapo zote 720 zimeonekana hazina maambukizi

Katika visa hivyo 43, Waganda ni 15, 9 ni Wakenya na 4 ni raia wa Eritrea ambao hao wamegundulika katika mpaka wa Elegu. Wengine waliogundulika katika mpaka wa Mutukula ni Watanzania 5 na Mrundi mmoja

Aidha, kuna wengine waliogundulika katika mpaka wa Malaba ambapo 5 ni Wakenya, Waganda 2, Mrundi 1 na dereva mwingine 1 ambaye uraia wake haujajulikana

Lakini pia, Jumla ya Wagonjwa 63 wamepona nchini humo tangu kuzuka kwa janga hilo
 
Mbona taarifa yako inaonekana kufurahishwa na watanzania kukutwa na maambukizi huko Uganda??
 
Sijasikia hata dereva mmoja kufariki dunia sababu ya corona

Hawa Uganda waache siasa kwenye vipimo
 
Back
Top Bottom