Visa vipya zaidi ya 5,000 vya maambukizi vyaripotiwa nchini Urusi

Suley2019

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2019
Posts
2,203
Reaction score
5,610
Idadi ya watu walioambukizwa rasmi virusi vya Corona nchini Urusi imefikia 68,622, baada ya kuripotiwa visa vipya 5,849 vya virusi hivyo, ikilinganishwa na Alhamisi, mamlaka ya afya nchini Urusi imebaini.

Watu sitini zaidi wamefariki dunia kutokana na ugonjwa wa Covid-19, na kufikisha idadi ya vifo vilivyothibitishwa 615, mamlaka hiyo imeongeza.

Hivi karibuni Rais wa Urusi Vladimir Putin alisema kuwa hali ya Corona nchini humo inaelekea kubaya.

"Tunaona kuwa hali inabadilika kila siku na kwa bahati mbaya inazidi kuwa mbaya. Idadi ya wagonjwa inazidi kuongezeka, haswa idadi ya wale walio na hali mbaya inazidi" alisema.

Putin, ambaye hivi karibuni alifanya tathmini juu ya ugonjwa wa Covid-19 katika mkutano wa baraza la mawaziri uliofanyika kwa njia ya video, alisema kwamba hali katika nchi yake inazidi kuwa mbaya, lakini hatua walizochukuwa kuudhibiti ugonjwa huo zinandelea kufanya kazi.

Rais Vladimir Putin alibaini kuwa, ikiwezekana, vifaa vya jeshi pia vinaweza kutumiwa kupambana na janga hilo, ambalo Umoja wa Mataifa ulisema linatishia ulimwengu.
 
Tuendelee kujikinga kwa kunawa mikono kwa sabuni na maji yanayotiririka pia tujifukize kwa maji yenye dawa mchanganyiko za asili, bila kusahau kuvaa barakoa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hii Corona imekomaa na wazungu kinoma,halafu wazungu wameshidwa kujitibu ndoo basi sisi tumekata tamaa.kwa dawa zetu hizi hizi za kienyeji tutizibiti kwa kuwa MUNGU katupa ngozi oji tutatoboa tuu bila shida

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Vifaa vya jesh vinatumika vip?

Back
Top Bottom