Visababishi vikubwa vya Ajali vya kuzingatia

Visababishi vikubwa vya Ajali vya kuzingatia

geranteeh

JF-Expert Member
Joined
May 21, 2015
Posts
268
Reaction score
646
Habari zenu wakuu. Hakika tunaanza wiki na pia tunaelekea kumaliza mwezi huu wa pili na kikubwa ni kushukuru Mungu kwa pumzi aliyotupatia kwani kwa masikitiko makubwa sana tumepoteza ndugu zetu wengi sana tangu kuanza kwa mwaka huu kikubwa tuombe Mungu sana atulinde na vyombo hivi vya moto tunavyoviendesha kila siku kwani ukiachana na sababu nyinginezo lakini pia Mungu pekee ndiye mwenye maamuzi ya mwisho katika uhai wetu na ndiyo maana kuna ajali inatokea ukiambiwa hii gari dereva katoka mzima unaweza shika kichwa. Leo ningependa tuzungumzie swala la ajali ili watu waweze kujifunza au wenye kujua waweze kupata ukumbusho. Takwimu na taarifa kutoka World Health Organization katika ripoti yao ya usalama barabarani kwa mwishoni mwa mwaka 2022 inasema kuwa kila mwaka takribani watu 1.35 Milioni hufa kwa ajali za barabarani kote duniani na ubaya zaidi wahanga wakubwa ni umri wa kuanzia miaka 5 hadi 29, Asilimia kubwa ni katika nchi zinazoendelea. Tukiangalia kwa Tanzania ajali za barabarani ni takribani asilimia 6.12% ya vifo vyote kila mwaka. Hakika takwimu hizi ziko juu sana. Kiufupi msingi wa huu uzi ni kipindi cha malumbano ya hoja nilichokiangalia wiki iliyopita hakika kuna vitu vingi sana vilinifanya niamue kutumia kalamu yangu angalau na wengine wajifunze huenda mtu akaokoka kutokana na bandiko hili. Yes nilitishika nilipogundua kwamba asilimia 90 ya ajali zote ulimwenguni hutokea katika nchi zinazoendelea na hasa Afrika Kuna vitu vingi sana viliongelewa lakini ili nisipoteze muda naomba nijaribu tu kuongelea vitu ambavyo tunaweza kujikinga navyo pindi tunapoendesha vyombo vya moto sisi kama sisi kwani najua kuna mtu anaweza kusema Miundombinu pia ni sababu ni kweli na yuko sahihi kabisaa ila wakati tunasubiria hili la miundombinu kutatuliwa je wewe kama mtumiaji wa chombo cha moto unajikinga vipi kwani maafa hayasubiri mtu pia mamlaka ina jukumu au lawama zake ila kwa leo naomba nijikite katika sisi binafsi kama watumiaji wa vyombo hivi vya moto moja kwa moja.

1. Uendeshaji mbaya
Naposema uendeshaji mbaya kuna vitu vingi sana vinaingia humu ndani lakini itoshe kusema kwenye swala la uendeshaji mbaya vijana ndio wanaoongoza na hii haijalishi kwa watu wanaopewa elimu au wasio na elimu kwa maana kusomea kwenye vyuo mbalimbali. Uendeshaji mbaya ni swala binafsi. Hakuna mtu wakukupangia mwendo wa kuendesha hasa kwa magari madogo ambayo kwa nchini kwetu hakuna limit ukitoa kwenye vibao vya mwendo yani maeneo yenye muingiliano wa watu. Tunaishi katika dunia ambayo kwa vijana wengi kuendesha kasi ni sifa wenyewe wanaita kumaliza kisahani. Binafsi siamini kwamba Tanzania tuna barabara ambayo inakuruhusu uendeshe 180 bali ni tunalazimisha tu. Kuna watu watapinga kwamba mwendo kasi si sababu lakini nikukumbushe tu kadiri gari yako mwendo unaoongeza ndipo madhara makubwa zaidi huongezeka pindi itakapotokea ajali. Madhara anayoyapata mtu akiwa speed 120 ni tofauti na yule wa 80km per hour.
Lakini hapo hapo kwenye uendeshaji mbaya ukiachana na speed huwa naamini kwamba udereva ni hesabu ambayo pale unaposhindwa kuipiga vema na kwa wakati sahihi matokeo yake ni kukugharimu maisha au hasara nyinginezo mfano mzuri ni hesabu wanayopiga watu wanaopita na red light hasa bodaboda ambayo pia ni uendeshaji mbaya wakifanikiwa wanapita lakini wakifeli huwa majanga. Lakini pia unatakiwa ujue ni wapi pa ku overtake na ni wakati gani wa ku overtake hata kama ni sehemu inayokuruhusu ku overtake ila hesabu yako ikikaa vibaya basi umekwenda na maji kiufupi matumizi mabaya ya hesabu zako unapokua barabarani na kuchukulia kila sehemu ni ya kufanya mahesabu inakuweka katika kundi la uendeshaji wa hatari sana wa kugharimu wewe na watumiaji wengine wa vyombo vya moto.

2. Kutokufuata Sheria za Usalama Barabarani.

Kwa uzoefu wangu hii ni sababu moja kubwa kama si ya pili inayosababisha ajali nyingi sana nchini kwetu. Katika vitu naviamini barabarani ni alama hizi hata kama sehemu ni nyeupe lakini kama hainiruhusu ku overtake sitofanya hivo abadani. Ajali nyingi hutokea kwa watu kuendesha kwa mazoea na kuamini mawazo binafsi kuliko alama zilizopo. Sawa wewe ni mzoefu katika barabara husika lakini kumbuka huna uhakika na uzoefu na elimu ya watumiaji wengine mfano usitegemee feva ndogo ndogo kwamba ninapoipita hii gari hata likitokea la kutokea basi atanisaidia kwa kupunguza mwendo au gari ya mbele yangu atatanua au kupunguza mwendo hapo ni sawa na kubeti maisha yako na hii Hufanywa sana na madereva wa mabasi ya mkoa au wa vyombo vya serikali na vyombo vya usalama (hapa namaanisha wasio na official privileges kama ving'ora) Udereva huwa hatuendeshi kwa mazoea, Sifa au kubeti hakika ukinusurika utakuwa na mengi ya kuelezea ikiwemo kujisifia au kushukuru Mungu kwa kukuokoa lakini ikitokea umefariki wazungu wanasema "Dead man tell no tales" hakuna second chance kwenye maisha ukilijua hilo daima utafata sheria na alama za barabara japo kwa bahati mbaya vijana wengi wanakufa kutokana na vipengele vya speed na kutofata alama za barabara.

3. Ukosefu wa Elimu kwa ujumla kwa watumiaji wa miundombinu ya barabara.
Hakika hapa siingelei waendesha vyombo vya moto tu bali ni wote wanaotumia miundombinu ya barabara naweza kukupa mfano mdogo tu. Serikali imejitahidi sana kujenga vivuko vya waenda kwa miguu hasa katika maeneo ambayo yana muingiliano mkubwa wa watu hapa namaanisha vijiji, shule au maeneo yenye shughuli za kiuchumi kama masoko na viwanda lakini ushawahi kujiuliza ni wangapi wanavuka kwenye vivuko? Yani mtu unakuta kivuko kiko hatua tano mbele yake lakin anaamua kuvuka anapoona panafaa, Okay achana na hilo huwa ni mara ngapi tunaona TANROADS wanaweka hadi mabango ya watu kutoendesha chughuli zao kwenye eneo la barabara lakini mtu unakuta kajenga banda lake chini ya hilo bango? Ni madereva wangapi wanaomiliki leseni wanajua sheria za barabarani? Tukiachana na mamlaka sisi kama sisi hata kama una leseni ya kuletewa basi unashindwa hata kuangalia video mbalimbali au kusoma vitabu mbalimbali vinavyohusu sheria na alama za barabara kwakweli ajali nyingi husababishwa na watu wasio na elimu ya usalama yani mtu akijua kuendesha gari anajua imeisha hakuna kingine trust me ukosefu wako wa elimu utakuja kukusababishia majanga makubwa tu wewe na wapendwa wako jaribu kuchukua hatua kwa kujifunza alama na sheria mbalimbali za barabara hata kwenye mtandao.

4. Sababu nyinginezo kama vile Hali ya hewa, Kutokuzingatia mifumo ya usalama, Ulevi na matumizi ya simu.

Kwa upande wa hali ya hewa kuna sehemu kama vile same ni sehemu ambazo kunakuwa na upepo mkali sana hasa nyakati za usiku yani usipokua makini trust me ajali utapata hili naongea kwa uzoefu. Kabla ya mwaka jana mwezi wa kumi hiki kipande cha same nilikua naona zile alama za upepo mkali lakini hayakuwahi kunikuta mpaka mwaka jana saa tano usiku narudi dar nilikua naendesha Alphard na tulikua watu kama kumi. Kiufupi nilikua speed kama sabini lakini ule upepo ulipotokea hta sijui yani gari nili lose control lakini mbele sikuwa naona kitu ni vumbi tupu sasa imagine kungekua na gari mbele yangu ingekuaje nashukuru Mungu nilitoka salama yani mpaka kesho naheshimu alama za upepo mkali unakatiza nikiiona naenda chini ya 60 hilo eneo. Lakini kuna ishu kama mvua na ukungu ambapo kuepukika kwake ni kujitahidi kuwasha taa na kwenda mwendo wa polepole au ikiwezekana egesha gari yako pembeni mpaka hali itakapoisha.
Katika upande wa kutozingatia mifumo ya usalama hapa ni swala Kutofaa kofia ngumu kwa madereva na abiria wa pikipiki wengi tunapuuzia hili mpaka yakitukuta lakini kwa wenye magari hakika swala la kuvaa mkanda ni ugonjwa wa taifa. Mara nyingi napopanda mabasi ya mkoa huwa najikuta ni mwenyewe ndo nimefunga katika majirani zangu yani hadi itangazwe na dereva au askari aingie kukagua yani saa nyingine natamani kungekua na video hata za kutengeneza za ajali zenye kuendana na uhalisia ili watu wajue madhara ya kutotumia hizi safety gears.
Mwisho kabisa ni swala la ulevi na matumizi ya simu. Vijana wengi tunawapoteza kwa uendeshaji huku wamelewa yani gari inachukuliwa kama chombo tu cha kawaida. Marehemu hasemwi lakini kuna mifano ya ajali kama mbili za hivi karibuni zinazohusu vijana ambao walilewa wakapata mzinga na hata maji hawakuomba lakini nisingeoenda kuziongelea ila kwa wenye tabia hii hakika hizi ajali ni reference kubwa sana na binafsi nachukia mtu akiendesha amelewa kwani athari zake huwa zinawapata sana watumiaji wengine mfano kuacha njia kwa kushindwa kuimudu gari au kuwadhuru unaowaendesha. Matumizi ya simu ukiwa umelewa sote tunajua athari zake lakini nimalizie kwa kusema amini kwamba "Chombo cha moto usipokiheshimu basi iko siku kitakushikisha adabu".

Imeandikwa na Mgaya
 
Ukitaka kujua umuhimu wa alama za barabarani endesha gari usiku, nimeendesha Sana usiku ingawa kuna risks hasa Kwa malori na mabus Ila unakuwa umepunguza safari yako.
Kwa mfano kipande cha DAR - MORO hapa kuna madereva vichaa wanaovertake mpaka kwenye Kona Kali mpaka unashangaa...kitu kingine ni michoro ya sakafuni(lami) hapa madereva wengi hawajui kusoma
 
".. Alphard na tulikua watu kama kumi.. "
Hii unaiweka kwenye kundi gani hapo juu kama chanzo cha ajali...!!!?
Mkuu wangu nilikua naelezea kuhusu situation ya mazingira ya hali ya hewa ambayo ilinikuta ya upepo mkali ulioambatana na vumbi na nimetaja hadi idadi ya watu tuliokuwemo so mtu aweze ku imagine uzito gari iliyokuwa nayo but mwisho wa siku upepo uliweza kunichota nakunitoa kwenye balance until nliposimama kwa pembeni. Then imagine uko na gari ndogo like ist na may be mko mtu moja au mbili ndani huu upepo utakufanyaje na may be upo speed 120[emoji3][emoji3]
 
Ukitaka kujua umuhimu wa alama za barabarani endesha gari usiku, nimeendesha Sana usiku ingawa kuna risks hasa Kwa malori na mabus Ila unakuwa umepunguza safari yako.
Kwa mfano kipande cha DAR - MORO hapa kuna madereva vichaa wanaovertake mpaka kwenye Kona Kali mpaka unashangaa...kitu kingine ni michoro ya sakafuni(lami) hapa madereva wengi hawajui kusoma
Sure mkuu alaf kuna kipande cha moro dodoma usiku wa manane kuna kama kipori fulani hivi cha dumila kunakuwa na lori kama zote na jamaa wa malori ni kama wamejimilikisha hiko kipande wanaendesha wanavojiskia
 
Mkuu wangu nilikua naelezea kuhusu situation ya mazingira ya hali ya hewa ambayo ilinikuta ya upepo mkali ulioambatana na vumbi na nimetaja hadi idadi ya watu tuliokuwemo so mtu aweze ku imagine uzito gari iliyokuwa nayo but mwisho wa siku upepo uliweza kunichota nakunitoa kwenye balance until nliposimama kwa pembeni. Then imagine uko na gari ndogo like ist na may be mko mtu moja au mbili ndani huu upepo utakufanyaje na may be upo speed 120[emoji3][emoji3]
Sehemu yoyote ile utakayokuta kibao cha onyo au tahadhari, tembea spidi chini ya 50kmph!!
 
Sure mkuu alaf kuna kipande cha moro dodoma usiku wa manane kuna kama kipori fulani hivi cha dumila kunakuwa na lori kama zote na jamaa wa malori ni kama wamejimilikisha hiko kipande wanaendesha wanavojiskia
Kuanzia kwa Makunganya mpaka unafika dumila huwa ni kama kuna down uchwara hivi, wenye malori huwa wanajitungua vibaya sana!

Baada ya dumila wanaanza mipando mpaka wafike kiyegeya..

Wakati huohuo kutoka kiyegeya mpaka unafika dumila ni down za kutosha, hapo pia wanajitungua vibaya sana!!

Hayo maeneo yanahitaji umakini wa hali ya juu sana, kosa dogo sana linaweza kuleta madhara makubwa mno.
 
Kuanzia kwa Makunganya mpaka unafika dumila huwa ni kama kuna down uchwara hivi, wenye malori huwa wanajitungua vibaya sana!

Baada ya dumila wanaanza mipando mpaka wafike kiyegeya..

Wakati huohuo kutoka kiyegeya mpaka unafika dumila ni down za kutosha, hapo pia wanajitungua vibaya sana!!

Hayo maeneo yanahitaji umakini wa hali ya juu sana, kosa dogo sana linaweza kuleta madhara makubwa mno.
Sure mkuu mi kuna siku nilipita usiku nikakutana na lori trela lake limepinda kama limakatika center bolt kichwa nilikipita vema tu kuja kutahamaki trela liko limeingia kidogo kwangu yani kwepa kwepa jamaa akaondoka na side mirror acha tu
 
Hakika, tatizo binadamu wa siku hizi ni wabishi sana...
 
Back
Top Bottom