Smartkahn
JF-Expert Member
- Jun 22, 2020
- 594
- 1,061
Peace||amani iwe nawe ✌🏾
Achana na ule upande wa pili wa Shilingi(sarafu), noti 💵 inapande tatu ukiachana na zile mbili zinazofahamika.
Upande wa tatu wa noti una picha au alama iliyowekwa na kudezainiwa kwa ustadi wa hali Ya juu kiasi kwamba unaweza usiitambue hiyo alama au usijue kama kwenye noti flani kuna picha ya buibui maisha yako yote.
Na maranyingi hizi alama huwa hazieleweki ziko upande upi wa noti hiyo, alama nyingine ni mpaka uinamishe au uelekeze noti katika mwanga flani ndio zinadhihilika.
Sasa kila nchi ina Fedha yake na hizi alama kitaalamu; banknote, zinatofautiana kati ya nchi na nchi pia thamani ya noti na noti.
Moja ya sababu ya kuunda banknote ni kuzuia utengenezaji wa Fedha bandia.
Hii ni intro ya uchambuzi wa siasa za kikanda na intelligensia nyuma ya migogoro ya kisiasa katika kanda mbalimbali....
Subiri muendelezo.
Karibu.
Kujazia nyama kidogo kwa vielelezo.
Katika noti ya dola 1 kuna buibui, kwa wenye noti ya dolla unaweza ukachunguza.
Hii hapa chini ni noti ya CANADA 🍁 Wanasema kuna taswira ya devil shettani kwenye nywele za Malkia
Unaweza ukaongezea na wewe alama unayoijua ambayo imejificha katika noti fedha ya nchi yoyote.