Vishoka wakithiri ofisi za umma

Vishoka wakithiri ofisi za umma

Mwizukulu mgikuru

JF-Expert Member
Joined
Oct 21, 2021
Posts
5,715
Reaction score
13,739
Gazeti la Mwananchi limeripoti kuwa, ofisi za umma zimesheheni vishoka, na hii imekuwa ikijidhihirisha hasa kwenye mambo ya ajira.

Ajira zinatangazwa kwa mfano TAMISEMI au Utumishi lakini kuna watu wanaambiwa leta vyeti na kiasi flani cha pesa halafu tulia wewe utapigiwa simu tu au utalikuta jina lako kwenye notice board.

Ombi langu ni kuwa, ni muda mzuri sasa serikali ya Watanzania kuwashughulikia vishoka. Madhara yapatikanayo kwa kuwepo vishoka kwenye ofisi za umma ni kama ifuatavyo:

  • Kumnyima haki na nafasi aliyesahihi na kumpa asiyesahihi kwa sababu tu asiyesahihi ana ukaribu na kishoka.
  • Kuleta urasimu katika baadhi ya mambo muhimu.

kwa leo niishie hapa.
 
KWA MFANO ARDHI,MATAPELI YANAPOFORGE HATI YA MTU SHUGULI HII HUCHUKUA WIKI TATU TU,HATI HUWA IMETOKA,SASA WEWE AMBAYE UNAFUATILIA HATI YAKO KIHALALI ITAKUCHUKUWA MPAKA MIEZI 6,MATAPELI NA VISHOKA SIELEWI WANATUMIA PRINCIPLE GANI,YAANI JAMBO HALALI HAPO ARDHI NI SHIDA KWELI.
 
Ila wanasaidia kwa nmna fulani kuharakisha mmbo..ukiwatumia vzr mana wengi wana channel kubwa na viongozi waandamizi wa serikali na chama.

#MaendeleoHayanaChama
Haya ndio mambo tusiyoyataka, wanasaidia huku wakiumiza watu wengine. Hebu tuwe taifa la watu wanaojielewa, vishoka na principles zake ni kwa ajili ya mataifa yasiyojielewa, yasiyofuata taratibu...
 
KWA MFANO ARDHI,MATAPELI YANAPOFORGE HATI YA MTU SHUGULI HII HUCHUKUA WIKI TATU TU,HATI HUWA IMETOKA,SASA WEWE AMBAYE UNAFUATILIA HATI YAKO KIHALALI ITAKUCHUKUWA MPAKA MIEZI 6,MATAPELI NA VISHOKA SIELEWI WANATUMIA PRINCIPLE GANI,YAANI JAMBO HALALI HAPO ARDHI NI SHIDA KWELI.
Kumuondoa Lukuvi wizara ya ardhi lilikuwa kosa kubwa sana. Samia alitukosea sana. Sasa hivi hati imekuwa shida sana kupata. mambo yanaharibika na kuvurugika kila uchao
 
Back
Top Bottom