'Visit Tanzania', Ubunifu mwingine kutoka kwa Barbra Gonzalez

'Visit Tanzania', Ubunifu mwingine kutoka kwa Barbra Gonzalez

kinje ketile

JF-Expert Member
Joined
Dec 12, 2015
Posts
5,089
Reaction score
9,664
Wanasimba na Watanzania kiujumla ni kama tumepitishwa kwenye mlolongo wa matukio kadhaa kutoka klabu yetu andamizi kwa muda mfupi.

Kwa lugha iliyokuja na meli matukio haya tungeita 'Surprises. Mara Simba Super Cup na sasa Visit Tanzania. Ukiangalia bila kuweka ushabiki yote ni Ubunifu unaohitaji utulivu fulani wa akili.

Kikubwa kingine ni timely approach ya kila Ubunifu. Kumbe Tz wa mama wenye uwezo wapo wengi ie Samia Suluhu, Tulia Ackson na sasa kwenye soka anajichomoza nguli mwingine Barbra Gonzalez CEO wa Simba.

Aah pokea pongezi mama!
 
Huyu ananikumbusha wa mama wengine walioacha alama...Kwa uchache marehemu Bibi Titi, Bi Kidude Huyu alitumbuiza,Gertrude Mongella nafikiri bado yu hai, na wengine wengi. Ubunifu anaouonyesha siku moja atawafikia na kuacha alama...! Tumuombee
 
Gertrude Mongela amefanya nini?Huyu mbona kama yuko overrated?
Bora ungesema marehemu Mama Gertrude Lwakatare
Huyu ananikumbusha wa mama wengine walioacha alama...Kwa uchache marehemu Bibi Titi, Bi Kidude Huyu alitumbuiza,Gertrude Mongella nafikiri bado yu hai, na wengine wengi. Ubunifu anaouonyesha siku moja atawafikia na kuacha alama...! Tumuombee
 
Hivi huyu mama ni mtanzania?

Ndiyo tatizo la kutoifahamu Tanzania. Kuna waTanzania wenye majina ya ukoo Fernandez, Dourado, De Souza, Da Silva, Carvalho,Figueiredo, Lobo, Mendez , Gonzalez , Pinto, Rebello, Rodriguez, Zapata n.k

Ni waTanzania wenye asili ya ki- Goa. Bila kusahau wenye asili ya kiGiriki, Gujarat, Shirazi, Nubi, Zulu, Sukuma, Nyamwezi, Omani , Gogo n.k

22 Apr 2016
Miongoni mingi iliyopita, mababu zao walitoka eneo la Goa, India na kuhamia Tanzania. Wamezaliwa nchini Tanzania na hata wakienda Goa huenda huko kama wageni.

Source : BBC news Swahili
 
Back
Top Bottom