Candid Scope
JF-Expert Member
- Nov 8, 2010
- 11,897
- 6,925
Mbunge wa Jimbo la Micheweni, Bw. Haji Khatibu Kai (CUF) alipendekeza kuwa kuvunjwa kwa muungano kwa kuwa hakuna uwiano katika mambo mbalimbali yanayofanywa na serikali. Alisema kuwa serikali haikueleza ni kero ngapi mpaka sasa zimeshughulikiwa hatua inayowafanya Wanzanzibari kuwa nyuma ikilinganishwa na wabara, hivyo akaomba kuwa kama Zanzibar imeonekana ni mzigo, basi muungano huo uvunjwe ili uundwe upya.
Naye Mbunge wa Magogoni, Bw. Kombo Khamis Kombo (CUF) alisema kuwa kumekuwa na uwiano usiokuwa sahihi katika mambo mbalimbali ambapo alitolea mfano uteuzi wa mabalozi katika nchi mbalimbali. Alisema kuwa mpaka sasa mabalozi wanaotoka Zanzibar ni wanne tu ambao wako katika nchi za Kiarabu huku idadi kubwa ya mabalozi wakitoka bara hivyo akaomba kuwepo uwiano katika teuzi mbalimbali.
Alisema kuwa serikali ina wizara 26, kati ya hizo sita tu ndizo za muungano, lakini mambo mbalimbali ambayo si ya muungano yamekuwa yakitengewa fedha hivyo akahoji usawa katika masuala hayo .Alisema kuwa kama kuna nia ya dhati ya kutatua kero za muungano ni vyema Waziri Mkuu akalisimamia vyema suala hilo ili kurejesha imani ya Wazanzibari.
Majira