Salary Slip
Platinum Member
- Apr 3, 2012
- 49,390
- 152,301
Kama umesoma historia ya nchi hii hasa katika mapambano au vita vya kupigana na mkoloni, bila shaka utakuwa umesoma na habari ya Mzee Kinjekitile Ngwale, kiongozi alieongoza watu wake katika kupambana na mkoloni ingawa alinyongwa na wakoloni wa kijerumani mwaka 1905 na kuacha vita ya maji maji(1905-1907)inaendelea (kwa kumbukumbu zangu).
Umaarufu wa Mzee Kinjekitile Ngwale unatokana na kuwaaminisha askari wake kuwa dawa ya maji maji aliyowapa ingegeuza maji risasi za wakoloni, na hivyo wangeshinda vita ile kitu ambacho hakikuwa sahihi.
Katika vita ya kupambana na corona duniani, naona bado wako viongozi wenye falsafa za kina Kinjekitile Ngwale za kuwaaminisha watu wao kuwa wataishinda corona kwa maombi, kujifukizia,watu kujenga immunity na mambo ya aina hiyo ikiwemo kukata chanjo badala ya kuwashauri watu wao wachukue tahadhari huku wengine wakiwaaminisha watu kuwa ugonjwa huo haupo kabisa katika nchi zao..Ajabu sana!
Binafsi naona viongozi wa aina hii ni kina Kinjekitile Ngwale wanaoishi katika karne ya 21 lakini wakiwa na mbinu za kina Kinjekitile walioshi karine ya ishirini.
Kama ambavyo Kinjekitile alisababisha maafa makubwa kwa askari wake waliouwawa na wengine kujeruhuhiwa na risasi za mkoloni, ndivyo ambayo baadhi ya watawala duniani leo hii wanaweza kuwaponza raia wao wakadhurika na huu ugonjwa kwa kuwaaminisha vitu ambayo kisayansi havijathibitika katika kukabiliana na huu ugonjwa.
Hivyo, watu wajiepushe na kina Kinjekitile wa dunia ya leo katika mapambano dhidi ya huu ugonjwa unaoisumbua dunia leo hii vinginevyo wataangamia kama askari wa Kinjekitile.