Je kwa mtindo wa kufutia waganga wote wa jadi leseni zao za kufanya kazi ya ujuzi wao katika kile ambacho kinaitwa 'kupambana na vita dhidi ya mauaji ya Albino) kuna uwezekano wa siku chache zijazo kwa Waziri Mkuu kutangaza kufutia leseni wahasibu wote wa serikali kwa sababu ya wachache ambao wanajihusisha na vitendo vya kifisadi?
Nini/nani atamzuia?
Hapa kwa mtazamo wangu ni kwamba huyu PM kakurupuka, tena karupuka kutoa agizo hili. Cha kujiuliza hapa ni je hiyo serikali inajua ni waganga wa jadi wangapi wana leseni za kazi yao? Na je wana zi renew wapi hizo leseni? na wanalipa kodi kiasi gani katika mapato yao? haya yakiwekwa wazi basi tujadili kuwafutia leseni.
1. Nijuavyo mimi kule vijijini ndanindani ambako Hospitali zipo Km 150 kutoka katika makazi yao wengi hutumia mitishamba katika kujitibu na miti hiyo hupendekezwa na waganga hao hao wa jadi ambao wengine hata leseni hawaijui ni kitu gani.
2. Kabla ya kutoa tamko hili PM angehakikisha kwanza serikali inajenga hospitali kwa wastani wa umbali wa KM 3 nchi nzima kwanza. Hapo ndipo angeweza kutoa Tamko lake hilo. Hili linanikumbusha enzi za Sumaye alipotoa agizo la kwamba akikuta wauza mchicha wa magomeni michicha yao ya kijani wamueleze maji wanatoa wapi wakati kuna shida ya maji Dar, baada ya kupiga marufuku umwagiliaji wa mchicha (Akapachikwa nickname: ZERO).
3. 99.9% ya wanasiasa ni wateja wakubwa wa waganga wa kienyeji hasa katika kusaka vyeo na ushindi. Sasa kuwapiga marufuku kufanya kazi zao hadharani ni kuwatia mjaribuni waheshimiwa na Pinda akiwa mmoja wapo. Nani asiyejua Bunge likianza pale Dodoma mji hujazwa na hawa wataalam wa Science ya kuruka kwa ungo?.
4. Serikali pamoja na kuwa na vyombo vya dola vyenye wataalam waliosomea pale CCP na kwingineko wameshindwa kutengeneza network ya kuwanasa hawa wauaji wa Albino?, mbona ni aibu sana kwa Nchi? ina maana hawa wauaji wanatechnolojia kubwa kuwazidi polisi? au Polisi wanaogopa nao kushushwa mishipa?, na kama wanaogopa je wale watakaoendelea kufanya shughuli zao za kiganga watakuwa na ubavu wa kuwakamata?.
5. Serikali imeshindwa kazi na kuwatupia mpira wananchi kwa kisingizio cha kufuta vibali vya waganga wa jadi na kuwataka wananchi wawaangalie waganga je, waheshimiwa kuanzia Rais, PM mawaziri wabunge na viongozi wote nao wapo tayari kuwataja waganga wao wa Jadi?. Basi waanze kutoa mfano wao kwa kuwaanika kabla wananchi nao hawajafuata mkondo. vinginevyo hii ni Ze Komedi.
Hoja ya mwanakijiji nilivyoielewa ni kwamba kama suluhisho la kupiga vita wauaji wa albino ni kufuta leseni za waganga wote kwa sababu miongoni mwao wapo wanaelekeza mauaji basi ni kweli na Wahasibu nao wafutiwe kwa sababu miongoni mwao wapo wanaoendekeza UFISADI, Nafikri hapo PM na washauri wake wameenda "Chaka" au wamekula "Kasa".