Eliawizy
New Member
- Jun 23, 2013
- 1
- 3
MWANDISHI : JOSEPH ELIEWAHA MSUYA
BARUAPEPE : josepheliewaha@gmail.com
ANWANI : P.O.BOX 104855, DAR ES SALAAM
SIMU: 0655 047 344 AU 0768 227 510
VITA INAYOPIGANWA NDANI YAKO:
Vita ni mgongano au mabishano yanayotokea baina ya pande mbili au zaidi. Vita husababishwa na kutoelewana/kutoafikiana katika maswala kadhaa yanayogusa pande hizo, hivyo hupelekea kuharibika kwa mahusiano.
Baada ya kutoelewana pande moja huamua kutatua tatizo au mgogoro walioupata kwa njia ya nguvu,. Upande mwingine pia hujibu mapigo hayo kwa njia hiyohiyo hivyo hupelekea maangamizi kwa pande moja au zote mbili katika kipindi hicho.
Vita husababishwa na Kugombea Vitu mbalimbali vyenye thamani kama Mali, Mawazo, Biashara, Kampuni, Ardhi, Nyumba (Jengo), Wanyama, Mahusiano, Watoto, Uongozi na mambo mengine yafananayo na hayo.
Zipo Vita za aina nyingi katika ulimwengu wetu wa leo, mfano wa vita hizo ni baina ya Mtu na Mtu, Familia na Familia, Koo na Koo, Kabila na Kabila, Jamii Fulani na Jamii Fulani, Taifa moja na Taifa linguine, Bara moja na Bara lingine.
Pia zipo Vita za Wanyama au Viumbe hai na kundi kwa umoja hadi makundi.Vilevile ipo Vita ya ndani ya Mtu ambayo hutokana na mgongano wa Fikra au mawazo yake binafsi.
Hii ndiyo Vita hasa niliyopanga kukuelezea ndugu msomaji. Vita hii hutokea ndani ya Mtu pale anapokua na mawazo mawili au Zaidi na kushindwa kufanya maamuzi/ uchaguzi wa nini kipewe kipaumbele Zaidi ya kingine.
Vita ya aina hii huwasumbua watu wengi na ndio vita ngumu zaidi kuwahi kutokea katika ulimwengu wetu wa leo. Vita hii hmpelekea mtu kuwa na msongo wa mawazo ambao huweza kusababisha magonjwa ya ufahamu kama Sonona na magojwa mengine ya akili ambayo husababisha kupungua kwa nguvu kazi ya mtu katika familia, taifa mpaka ulimwengu mzima kwa ujumla.
Mtindo wa Maisha yetu ya leo hupelekea watu wengi kukumbwa na aina hii ya vita inaua ndoto na vipaji vya watu wengi. Vita hii huanzia mbali tangu mtu hajazaliwa na huweza kuwatokea mzazi wa kike au wa kiume ama wote wawili kipindi walipopokea majibu ya kuwa watakua wazazi baada ya kipindi cha miezi tisa (9) ijayo.
Mzazi wa kiume anaweza kuanza kuwaza ni kwanini amepata Mtoto kipindi hicho, mwaka huo, atawezaje kumudu gharama za Mzazi mwenzie kabla na baada ya kujifungua, atawezaje kugharamia malezi, elimu na mambo mengine akilinganisha na kipato chake, ukubwa wa familia yake huku akikimbizana na mud ana maendeleo yake kwa ujumla.
Mzazi wa kike anaweza kupata vita ya ndani kutokana kutokana na kuachwa au kukimbiwa na mzazi mwenzie, hivyo naye huweza kujiuliza kuwa atawezaje kumudu peke yake au hata wakiwa wawili lakini uwezo wa chini, au hakutarajia/ hakupanga kwa kipindi hicho kuwa na mtoto (watoto) hivyo hupelekea ndani ya ufahamu wake kuwa na msongo mkubwa wa mawazo yanayokinzana na kushindwa kuamua nini cha kufanya kwa muda huo ili aishinde vita hiyo ya mawazo na kuendelea kuishi vizuri kwa amani na furaha wakati wote kabla na baada ya uzazi.
Vita hii huweza kusababisha madhara wakati wa ujauzito, kipindi cha kujifungua na hata kipindi cha kulea kwani hata malezi mazuri na malezi mabaya ni matokeo tu ya aidha kuishinda vita hii au kushindwa na mwishowe Mtoto ndiye mwathirika mkubwa zaidi.
Vita hii huendelea hata mtoto anapokua mpaka anapopata ufahamu wa kufanya maamuzi yake binafsi naye pia huweza kurithi au kuendeleza vita hii baada ya kupokea kutoka kwa wazazi au walezi wake au jamii (mazingira) yanayomzunguka.
Kuna Msemo wa Kiswahili husema, “Mtoto umleavyo ndivyo akuavyo”.
Ndiyo hasa mambo yanayowatokea watu wengi katika Maisha ya leo, kwani kupata kwao aina Fulani ya malezi hupelekea kuishi Maisha ya aina Fulani pale wanapofikia umri wa kujitegemea au kufanya maamuzi yanayohusu Maisha yao na watu wanaowazunguka.
Mtu akifikia umri wa ujana hadi uzee hupita changamoto mbalimbali ambazo huweza kusababisha vita/mgongano wa mawazo ndani ya ufahamu wake. Sababu mbalimbali husababisha Vita hii ndani ya ufahamu wake kutokea zinaweza kutoka kwenye malezi aliyoyapata pindi akikua, Aina ya Marafiki alio nao na ushawishi wao kwenye maamuzi yake, jinsia yake, Elimu yake, kazi yake, mazingira anayoishi, mahusiano yake na Maisha yake kwa ujumla yanavyoenda.
JINSI YA KUSHINDA VITA VINAVYOPIGANWA NDANI YA FIKRA ZAKO
1.) Kuwa na Malengo ya muda mfupi na Muda mrefu na jifunze kuwa na kipaumbele katika kutimiza malengo hayo. Watu wengi tumekua watu wenye mawazo kwasababu ya kuendesha Maisha yetu bila malengo, hii imepelekea kushindwa kufanya maamuzi sahihi hasa tunapopitia changamoto kwani tumekua tunakurupuka kufanya maamuzi juu ya Maisha yetu kwa ujumla. Kuwa na Malengo ya Masaa, Siku, Mwezi, Mwaka na Hata Miaka kadhaa kwamba unataka kufika sehemu Fulani, Weka kipaumbele kwa baadhi ya malengo ili uweze kufanikiwa kuyatimiza.
2.) Jenga ujasiri na msimamo wa kufanya maamuzi kwani Mwendesha Maisha na hatima yako ni wewe mwenyewe. Usipojiamini hutaweza kuamua na usipoamua hutaweza kuthubutu kufanya. Hatima ya Maisha yako inataka uthubutu na msimamo ambao huja kwa kukataa sauti inayokuogopesha au inayokwambia huwezi/utashindwa. Kwani hata walioshinda na kufanikiwa maishani walipitia kushindwa hivyo jiamini na ufanye.
3.) Jifunze kusamehe na kuachilia watu/mambo yaliyokusababishia msongo mkubwa wa mawazo. Kwani hata vitabu vya dini vinatuambia, Katika Biblia Mathayo 6 : 14 Kwa maana mkiwasamehe watu makosa yao, na Baba yenu wa Mbinguni atawasamehe ninyi” Ukisamehe watu moyoni mwako utaweza kuwa huru na kutoka kwenye mtumwa wa limbi la mawazo. Usisubiri Mtu akuombe Msamaha hata wewe, anza wewe kusamehe ili uwe huru.
4.) Kuwa na watu sahihi (marafiki) wa kukushauri katika kutimiza malengo yako. Jua kuwasoma watu kwani Maisha ya sasa wapo watu wengi wanaoweza kukuongezea vita ndani ya fikra zako hivyo pima na uchague mtu/ watu sahihi kushirikisha mambo yako au kuomba msaada pale unapokwama. Hata unapotumia ushauri wao na ukashindwa kufaulu, usivunjike moyo kwani hata "Roma haikujengwa siku moja" Msemo.
5.) Tenga muda wa kufurahi. Unaweza kutumia muda huo kuwa peke yako au na marafiki zako au na familia yako.
6.) Jifunze kuwa Mtu wa kumaliza mambo unayoyapanga au kuyaanza katika Maisha yako. Usikate tamaa katika kufanya mambo yako, kwasababu kadiri unavyokata tamaa na mara kwa mara kushindwa kutimiza malengo yako ndivyo hupelekea kuongezeka kwa vita ya kifikra. Lakini ukiwa mtu wa kuendelea kupambana juu ya ulichokianzisha iwe ni kazi, elimu, biashara, kampuni, Urafiki, Mahusiano utaweza kufika mbali na kufanikiwa.
7.) Mazoezi ya mwili huweza kuondoa Vita inayopiganwa ndani ya fikra. Mazoezi ya mwili hufungua akili na kuondoa msongo wa mawazo kwani hujenga afya ya mwili na akili kwa ujumla.
8.) Kuwa na Muda wa kupumzika. Unapopumzisha mwili wako baada ya kufanya kazi husaidia mwili kurudi kwenye hali yake ukiwa na nguvu za kutosha na utimamu mzuri katika kutimiza malengo yako. Muda wa Kufanya kazi fanya kwa bidii ila unapomaliza tenga muda mzuri wa kupumzika.
9.) Mtangulize Mungu katika Mambo yako. Hapa anza na Mungu hata unapoianza siku yako. Asubuhi uamkapo, Mkabidhi Mungu malengo na Ratiba yako. Mshukuru Mungu kwa unapopata na unapokosa, jifunze kuwa mtu wa dua na Muombe Mungu akuongoza katika kufanya maamuzi na kukuondolea Vita ya kifikra ndani yako.
Vita ya Kifikra (yaweza kukurudisha nyuma au kukudumaza katika kufanya maamuzi hivyo kupelekea kushindwa. tambua na funguka kutoka kwenye kifungo hiki cha mawazo kwa kujifunza na kufanya mambo haya kadhaa. Amua sasa kushinda vita hii ili uweze kuwa huru kiafya na kuweza kufanya mambo yatakayokuletea tija na maendeleo kwenye Maisha yako.
Asante kwa kusoma Makala hii na nina Imani umepata kitu cha kukusaidia kwenye kushinda vita ya kifikra.
[emoji2398] Haki zote zimehifadhiwa

Attachments
Upvote
3