Vita itakuwaje ikitokea USA na CHINA wakipigana

Vita itakuwaje ikitokea USA na CHINA wakipigana

krava

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2016
Posts
225
Reaction score
287
Wataalamu wa mambo ya vita tuambieni vita kati ya China na USA itapigwaje maana wako mbali sana maelfu ya kms

Je watatumia IBM intercontinental ballistic missiles au maana hata Yale mameli makubwa aircraft carrier yako vulnerable kuwa tagerted litazamishwa baharini soon likianza Ku move mfano Nimitz

Haya tukija kwenye madege yatatunguliwa tu yakianza kuingia kwenye air space ya adui askari wa miguu ndio kabisaaaaà haiwezekani eti infantry ya Beijing ikanyage mitaa ya Manhattan na kinyume chake sasa vita kati ya mataifa haya itapigwaje?

Kuhusu mrusi yeye tunamsogezea mavitu yote ulaya kuanzia vifaa mpk askari vita hebu wajuzi wa Vita tuambieni
 
Kilometa kutoka China hadi Marekani ni Kilometa zisizopungua 11,671 ambazo zinaweza kufikika kirahisi sana na hizi ndege za kivita kama ile B 2 ya Marekani. Kwa kawaida ndege inayoweza kwenda maili 560 kwa saa inaweza kuchukua Masaa 12 tu kufika.. Sawa na mwendo wa Basi kutoka Dar hadi Mbeya. Na pia Kuna Rocket rangers za kisasa kabisa ambazo zinaweza kusafiri kwa speed kubwa kuliko kawaida . Usisahau pia kua China na Marekani zina Nuclear powered Submarine zenye uwezo wa kusafiri umbali mrefu sana......In short vita itapiganwa majini,Nchi kavu na Hata angani
 
Mkuu krava, kama ninakusoma vizuri, ni kama unatilia maanani umbali kutoka pwani ya mashariki ya Marekani kwenda China ukikatisha bahari ya Atlantic halafu anga la Africa au Ulaya. Kama ni hivyo kumbuka kuwa U.S. wana vituo vya kijeshi vilivyotapakaa maeneo mengi. Kumbuka pia wamekuwa na harakati za kijeshi Afghanistan kwa miaka mingi na iko mbali nao pia. Kwa hiyo vituo hivyo viwe vya baharini au nchi kavu vitatumika, na kwa wachina vitakuwa target za mapema kabisa kushambuliwa. Lakini pia ikiwa kuna ndege za kiraia (abiria) zinatoka miji ya pwani ya magharibi ya marekani kama L.A., San Francisco, Seattle n.k. kwenda Asia kwa kukatisha anga la bahari ya Pacific, majeshi ya nchi hizo mbili hayatashindwa kufikia target zao kwa upande ule ambao ni mfupi zaidi. Hapa ukumbuke njia iliyotumia meli iliyosafirisha mabomu ya atomic yaliyotumika dhidi ya Japan mwishoni mwa WW2.
 
Obvious hawawezi kupigania Marekani wala China,wataangalia nchi ambayo hawamind vitu vdogo vdogo kama vita ,inaweza kuwa Congo au Sudan
 
Taiwan nadhani inaeweza ikatumika na mmarekani kama kituo chao cha kijeshi.. Jaribu kufuatilia mgogoro unaotokoka kati ya Taiwan na China kuhusu Bahari ya kusini(Southern sea). Kisha fuatilia nani anampa kichwa Taiwan,,,
 
Back
Top Bottom