Vita kati ya Mangi Meli na wajerumani huko Kilimanjaro

Vita kati ya Mangi Meli na wajerumani huko Kilimanjaro

Kanungila Karim

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2016
Posts
20,743
Reaction score
25,564
Na huko upande wa kaskazini wa Koloni la Wajerumani la Afrika ya Mashariki, Wachagga nao, chini ya Mangi (Mteni) Meli wa Moshi, walikataa katakata kutawaliwa na Wajerumani.

Katika jitihada za kutaka kuwatiisha Wachagga, serikali ya kikoloni ya Wajerumani ilipeleka jeshi la askari huko Kilimanjaro, lililoongozwa na Burlow akisaidiwa na Luteni Wolfrum. Jeshi hilo la Wajerumani lilishambuliwa na askari wa Mangi Meli waliolizingira kwa ghafla kutoka maoteoni.

Bwana Burlow, Luteni Wolfrum pamoja na askari wengi wa Wajerumani waliuawa. Askari wa Kijerumani walionusurika walirudi haraka Marangu, mahali ambapo makao yao makuu yalikuwa yamehamishiwa.

Baada ya kuunda jeshi jingine lenye nguvu.

Wajerumani walikusudia kwenda tena Kilinjaro kumpiga vita Mangi Meli aliyekuwa akikataa kuwekwa chini ya utawala wao. Safari hii jeshi hilo la Wajerumani lilitokea pwani kuelekea Kilimanjaro, liliongozwa na Gavana mwenyewe bwana Friedrich von Schele. Baadhi ya wamangi (Watemi) wa Uchaggani waliokuwa na uhasama na
 
Back
Top Bottom