ShyaRuwa
JF-Expert Member
- May 30, 2015
- 7,895
- 13,643
The Anglo-Zanzibar war, ilikuwa vita kati ya Zanzibar na Uingereza iliyotokea Ijumaa ya tarehe 27 August 1896.Hii ndio vita iliyodumu kwa muda mfupi zaidi hapa duniani, vita ilidumu kwa muda wa dakika arobaini na tano, 45 [inagawa machapisho mengine yanasema vita ilidumu kwa muda wa dakika 38, au 40].
Vita ilianza baada ya kifo cha Sultani Hamad bin Thuwaini aliyekuwa mshirika wa utawala wa kikoloni wa waingereza kilichotokea 25.08.1896. Baada ya kifo cha Sultani, 'mpwa' wa Sultani aliyeitwa Khalid bin Bargash (29) alitwaa madaraka, kitu kilichotafsiriwa kama mapinduzi ya kiutawala kwani wakoloni walipendekeza Hamud bin Muhammed awe Sultani ili iwe rahisi kushirikiana naye.
Serekali ya kikoloni ilimtaka Bargash aachie madaraka lakini alikataa na alijiwekea ulinzi wa kijeshi kuzunguka makazi yake ya kisultani.Kufuatia ubishi wa Bargash, wakoloni walikusanya meli tano za kivita baharini karibu na makazi ya Bargash.Pia waingereza walitoa msaada kwa watu waliokuwa watiifu kwa utawala wa kikoloni ili kupigana dhidi ya Bargash.Dakika za mwishoni kabla ya kuanza kwa vita, Bargash alijitahidi kufanya mazungumzo na waingereza kupitia kwa wawakilishi wa US visiwani Zanzibar lakini jitihada zake hazikufua dafu kwani saa tatu asubuhi ya tarehe 27.08.1896 waingereza walianzisha mashambulizi.
Bargash na jeshi lake hawakuweza kustahimili vishindo vya waingereza kwani walisarenda baada ya dakika 45 za mapigano.Bargash alitoroka kwenda kwenye 'ubalozi' wa kijerumani, waingereza waliwataka wajerumani wamrejeshe Bargash lakini haikutokea kwani tarehe 2 October Bargash alitorokea baharini kwenda Dar es Salaam.Bargash aliishi uhamishoni Dar es Salaam hadi alipokamatwa na waingereza mwaka 1916. Baada ya kukamatwa Bargash aliruhusiwa kuishi Mombasa hadi alipofariki mwaka 1927.
Waingereza waliitaka serikali ya Zanzibar kulipa gharama za vita.Inakadiriwa wazanzibari kati ya mia tano waliuawa na kujeruhiwa ili hali ni mwanajeshi mmoja tu wa kiingereza aliyejeruhiwa.